Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:59
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Akaunti zinazozingatia vita kwenye mitandao ya kijamii zinadai video inayoonyesha vikosi maalum vya Marekani vikiokoa ndege ya pili iliyokwama nchini Iran baada ya ndege ya kivita ya Marekani F-15E kudunguliwa Aprili 3, 2026.
Moja ya chapisho la Aprili 5, kwenye X, linasoma,
"Moja kwa moja kutoka kwa filamu ya vita. Usiku wa manane, vikosi maalum vya Marekani vinamtafuta rubani wa pili na kutua usafiri kwa ajili ya kumtoa lakini inakwama." Lakini huu ni uongo; picha zinatoka katika mazoezi ya kijeshi ya Julai 2024 katika jimbo la California.
Madai kama hayo yalienea kote X na Facebook, chapisho moja likidai kwamba picha kutoka kwenye video hiyo ilionesha Marekani ikikimbia kwenda kuokoa ndege ya F-15 iliyoanguka kutoka Iran."
Utakumbuka mnamo Aprili 5, Rais Donald Trump alitangaza kwamba vikosi maalum vya Marekani vilifanikiwa kumtoa mhudumu wa mfumo wa silaha ambaye alitoka kwenye ndege iliyodunguliwa Aprili 3 nchini Iran.
Lakini video inayosambaa mtandaoni sio video ya operesheni hiyo, kama inavyodaiwa. Kwa kutumia mbinu ya Reverse Image search, video sawia na hiyo ilichapishwa mwaka 2024, kwenye tovuti ya ulinzi ya Pentagon (DVIDS), na pia kwenye tovuti zingine rasmi za kijeshi.
Maelezo yake yalisoma: "Katika operesheni ya pamoja, walifanya oparesheni za kusambaza silaha na kuongeza mafuta katika Kituo cha Kitaifa cha Mafunzo, Fort Irwin, California, Julai 16, 2024. Klipu sawia na hizi kutoka kwa DVIDS zimepotoshwa mara kwa mara mitandaoni.
11 avril 2026
Swahili (generic)
9 Mo