Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:56
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Uhusiano kati ya DRC na Rwanda bado ni wa kusuasua. Hali hiyo hiyo inawahusu rais wa sasa wa DRC Felix Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila. Katika muktadha huu, picha na video zinazomwonyesha Kabila, zimekuwa zikisambaa mtandaoni mwezi Julai na Agosti zikiambatana na madai mbalimbali.
Picha inayosambaa kwenye X na Facebook inadai kuwa Kabila na Rais Paul Kagame wa Rwanda walikutana jijini kigali, pamoja na bilionea wa Marekani Bill Gates, ambapo waliafikiana kuhusu mipango ya kiuchumi na ya amani.
Chapisho hili lilizua shaka, na ukaguzi kwenye google lakini pia katika wavuti rasmi wa serikali ya Rwanda hatukupata matokeo yanayoambatana. Kwenye akaunti rasmi ya X ya ofisi ya rais wa Rwanda, tulipata picha hii—iliyowekwa mtandaoni tarehe 21 Julai 2026—inayowaonyesha Paul Kagame na Bill Gates na Kabila hayuko kwenye picha hiyo.
Baada ya kuchunguza picha hiyo, tuliona alama ya Gemini, yenye umbo la nyota, karibu na kifundo cha mguu wa kushoto cha Kabila. Hii inaashiria kuwa picha hiyo ilitengenezwa na akili unde, AI. Kabila hakukutana na Rais Paul Kagame wala Bill Gates wakati wa ziara rasmi ya Gates nchini Rwanda kuanzia tarehe 20 hadi 21 Julai 2026. Picha hiyo ni ubunifu wa AI.
Tukiwa bado na suala la Congo, Sasa tuchunguze video ya sekunde 10 ikidai kumuonesha Kabila akishuka kutoka kwenye gari. Video hii ilichapishwa kwenye mtandao wa TikTok ikidai kuonyesha Kabila akiwasili jijini Kinshasa tarehe 13 Agosti 2026.
Tulifanya utafiti kwa kutumia maneno muhimu kama vile "kuwasili, Joseph Kabila, Kinshasa, Agosti 2026" na hatukupata taarifa yoyote iliyoripotiwa na chombo chochote cha habari cha Kongo au cha kimataifa kinachogusia madai hayo. Hata sisi hapa RFI Kiswahili hatukuripoti kuhusu habari hiyo hata vyombo vingine vya Habari havikuwa na taarifa hii
Tuliendelea kuchunguza haabri hii kwa kutumia Reverse Image Search, tulipata video sawia na inayosambazwa, lakini hii ilikuwa na maelezo yanayosema: "Kenya: Joseph Kabila awasili katika eneo la mkutano na wapinzani wa Félix Tshisekedi jijini Nairobi." Iliwekwa mtandaoni mnamo Oktoba 2025.
Ilikuwa ni kongamano la kisiasa la siku mbili lililofanyika kuanzia tarehe 14 hadi 15 Oktoba 2025, jijini Nairobi, Kenya. Nakala moja ilichapishwa pia mtandaoni wakati huo na ilitumia picha hiyo hiyo pamoja na picha nyingine kutoka kwenye mkutano huo.
Tangu wakati huo, Kabila hajaonekana hadharani. Hakuna ushahidi unaothibitisha video inayoonyesha kuwasili kwa Kabila jijini Kinshasa mnamo Agosti 2026, video hiyo inayosambaa ilirekodiwa Oktoba 2025 jijini Nairobi, Kenya.
05 septembre 2026
Swahili (generic)
9 Mo