Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:54
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Tunaangalia ni video ya zamani yake rais wa Uganda Museveni inayohusishwa na maandamano ya mwezi uliopita nchini Kenya.
Maandamano nchini Kenya ya tarehe 7 Julai ya kuunga mkono demokrasia yalikumbwa na vurugu, uporaji na uharibifu wa mali. Baadaye rais William Ruto aliwapa polisi mamlaka ya kuwafyatulia risasi wahalifu miguuni kisha kuwafungulia mashtaka, badala ya kuwaua.
Kutokana na matukio haya, kuna vídeo moja nimeiona mitandoani ikidai rais wa UgandaYoweri Museveni akikosoa jinsi polisi wa Kenya wanavyokabiliana na waandamanaji.
Maandishi yaliyowekwa kwenye video ya Tiktok iliyochapishwa Julai 11, 2025 yalisema “Rais Museveni hajafurahishwa na polisi wa Kenya kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.
Maelezo yanayoambatana na chapisho hilo yanasema, "Museveni alimkosoa Rais wa Kenya William Ruto kwa ukatili wa polisi dhidi ya waandamanaji." Dai ambalo pia lilishirikiwa kwenye X na Facebook.
Hata hivyo, machapisho ya mitandao ya kijamii yanayodaiwa kumuonyesha Museveni akijibu matukio ya hivi majuzi nchini Kenya ni ya uongo. Video hiyo ni ya safari ya siku sita ya Museveni mwaka 2020 kuadhimisha mapambano ya ukombozi wa 1986.
Ili kuthibitisha video hiyo, matokeo yanatupeleka hadi klipu iliochapishwa awali na chombo cha habari cha Uganda NBS Television mnamo Januari 5, 2020.
Katika video zote mbili, rasi Museveni anaonekana akiwa amevalia mavazi yaleyale, akiwa ameshika fimbo moja, na amesimama nyuma ya vipaza sauti viwili vilivyofunikwa na kitambaa cha manjano. Hema la rangi ya chungwa pia linaonekana nyuma yake.
Kipindi hicho Museveni alikuwa ameanza safari ya siku sita iliyopewa jina la "Africa Kwetu" ya umbali wa kilomita 195 akifuata njia ambayo kikosi chake cha National Resistance Army (NRA) walichukua waliponyakua mamlaka mwaka 1986.
Rais Museveni alizungumzia swala hili tu wakati akiwaonya vijana wa Uganda dhidi ya kufanya maandamano kama hayo nchini mwao. Hata wiki hii alipokuwa Nairobi hajazungumzia hilo.
02 août 2025
Swahili (generic)
9 Mo