Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Katika mtandao wa X kuna video ya tangu Juni 30, ikidai kumwonesha rais wa DRC, Felix Tshisekedi, akimpiga teke kichwani mwenzake wa Zambia, Hakainde Hichilema.
Mchapishaji wa video anauliza swali, “Kwa nini marais wawili wanapigana hadharani.”
Mtumizi mmoja alisema “Hii si ukweli bali ni AI.” Mwingine akasema "Hii si kweli. Ukichunguza kwa makini, yule jamaa aliinua mguu wa kushoto na kupiga teke na wa kulia. Hii ni AI inatuchezea"
Chini ya saa 24, chapisho lilikuwa limetazamwa na zaidi ya watu laki 4 na kusambazwa zaidi. Wengi wakisema video hii imeundwa kupitia AI. Mtumizi mmoja akajibu "Eeh kuinua mguu wa kushoto kisha kupiga teke kwa kutumia mguu wa kulia". Mwingine alitoa tahadhari "Kabla mtu hajachapisha chochote, ni bora kujaribu kuthibitisha hilo. La sivyo, habari potofu ni uhalifu mkubwa."
Katika shughuli yetu ya kuhakiki, kwanza, ukiitazama video marais hawa wameketi bega kwa bega, kisha Tshisekedi anasimama kumpiga teke Hichilema bila yeye kutaka kujitetea na hapo anaanguka chini. Katika hali ya kawaida, ikiwa mtu anataka kukupiga, utataka kujikinga. Hii haijaonyeshwa kwenye klipu.
Tunaweza pia kuthibitisha kuwa video imetengenezwa na AI. Ni picha iliyochukuliwa na kutumia AI kutengeneza video. Picha hii ni ya Novemba 2021, wakati Hichilema na Tshisekedi walifanya mazungumzo mjini Kinshasa, kwa makubaliano ya kutatua vikwazo vya kibiashara.
Na vidokezo vya jinsi ya kujua video imeundwa kwa kutumia AI. Kwa makini angalia nyuso, macho, sikiliza sauti inayotumika na katika video hii, tunaona tu vitendo na hakuna sauti. Pia tafuta vitendo visivyo na maana kama vile Hichilema kukaa tu mtulivu kutokana na shambulio kutoka kwa Tshisekedi.
05 juillet 2025
Swahili (generic)
9 Mo