Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:59
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Katika mtandao wa Tiktok kuna video mbili zinazodai kwamba Uganda imerekodi mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mwezi huu wa Oktoba. Walakini video zote mbili ni za mwaka 2022.
Ya kwanza ni video ya Oktoba 10, ikimhusisha mke wa rais Janet Museveni ambaye ni Waziri wa Elimu na Michezo wa Uganda, akizungumzia virusi hivyo.
Madai sawa na hayo yalishirikiwa kwenye Tiktok Oktoba 12, yakiwa na chapa ya Bukedde TV na kichwa cha habari kilisoma: "Uganda imerekodi mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola. Watu 5 wamethibitishwa kufariki."
Katika ukaguzi wetu, tunapata kuwa video zote mbili ni za zamani.
Video inayomhusisha mkewe Museveni akizungumza kuhusu Ebola ni ya zamani, Novemba mwaka 2022, wakati akitoa miongozo ya usimamizi wa Ebola shuleni.
Vile vile, ile ya rais Yoweri Museveni, akizungumza kuhusu Ebola, video asili ilichapishwa na Bukedde TV mnamo 29 Septemba 2022. Madai kwamba Uganda ilirekodi mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mwezi Oktoba ni UONGO.
Pia tuliangalia kwenye wavuti na akaunti za wizara ya afya ya Uganda, kuhusu madai haya ya mlipuko wa Ebola Uganda mwezi huu na hatukupata.
Mwandishi wetu kutoka Uganda Kenneth Lukwago pia amezitaja video hizo kuwa za uongo.
17 octobre 2025
Swahili (generic)
9 Mo