Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:00
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Taarifa mitandaoni zinadai serikali ya Tanzania imepandisha umri wa kuolewa hadi miaka 30.
Mapema Mei 2026, madai yameenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba serikali ya Tanzania imeongeza umri wa chini wa kisheria wa kuolewa hadi miaka 30.
Maelezo yanayounga mkono madai hayo yanasema kuwa serikali imechukua hatua hii ili kuongeza tija miongoni mwa vijana.
Dai hili lilienea kwenye mitandao ya kijamii, mtumiaji mmoja ameandika “Hii italeta mabadiliko". Mwingine ameandika “Huu ni uongo” Umezipata wapi taarifa hizi ambazo ni kinyume cha sheria?”
Asasi za Kiraia nchini humo kwa sasa zinatafuta marekebisho ya kifungu cha Sheria ya Ndoa kinachoruhusu watoto chini ya miaka 18 kuolewa.
Katika hukumu ya kihistoria ya Julai, 2016, Mahakama Kuu ya Tanzania iliamua kuwa Sheria ya Ndoa lazima ifanyiwe marekebisho ili kuondoa tofauti kati ya umri wa chini wa kuolewa kwa wavulana na kwa wasichana.
Ni uamuzi uliokuja baada ya serikali kuweka hatua kali zaidi za kuhakikisha wasichana wa shule hawalazimishwi kuingia kwenye ndoa za mapema.
Wakati huo bunge lilikuwa limeharamisha mtu yeyote kuoa wasichana wa shule za msingi na upili, kosa ambalo mtu angehukumiwa miaka 30 jela.
Hata hivyo mwaka 2019, Mahakama ya Rufaa ilikubali uamuzi wa Mahakama Kuu kwamba wasichana au wavulana hawaruhusiwi kuolewa kabla ya kufikisha miaka 18.
Katika kuhakiki msikilizaji, hatujapata sheria au matangazo ya hivi majuzi yaliyoongeza umri wa chini kabisa wa kisheria wa kuolewa hadi miaka 30, kama inavyodaiwa katika machapisho ya mitandao ya kijamii.
22 mai 2026
Swahili (generic)
9 Mo