Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:55
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Malaria ni ugonjwa, unaosambazwa kwa kung'atwa na mbu jike aina ya Anopheles. Nchini Kenya, Taasisi ya Utafiti wa Matibabu (Kemri) ina jukumu la kufanya utafiti wa afya ikiwemo ugonjwa wa Malaria.
Mara nyingi maeneo yanayoathirika haswa nchini Kenya ni maeneo ya Magharibi, kule Nyanza na pwani ya Kenya. Sasa machapisho kwenye mitandao ya kijamii yanadai taasisi ya KEMRI inawatafuta watu 200 wa kujitolea kushiriki katika utafiti wa Malaria kwa malipo ya shilingi elfu 48,000. Ingati ukipiga hesabu hiyo ni kama dola ngapi za Marekani?
Hizi ni sawa na dola za Marekani 370. Sehemu ya moja ya chapisho kwenye Facebook na X inasema hivi
“Utafiti huo unawahitaji waliojitolea kukaa siku 24 hospitalini ili kupata malipo ya kila siku ya KSh 2,000 kwa kipindi cha utafiti. Jaribu bahati yako.”
Dai hili lilichapishwa kuanzia Juni 16 mitandaoni na kuvutia maelfu ya maoni. Mmoja kaandika “Ya ebola ikifika muniite.... watoto wangu lazima waishi katika utajiri
Mwingine alihoji “Malaria inaweza kuua ndani ya saa 24 isipotibiwa, ni lini binadamu katika nchi yetu walianza kuwa nguruwe wa kufanyiwa majaribio.
Mara moja tunaanza kuhakiki habari hii ya kupotosha kuhusu afya. KEMRI kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, waliweka wazi kuwa madai hayo yanayosambazwa ni ya uwongo.
Nasoma walivyoandika
“KEMRI inapenda kufafanua madai yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Taasisi hiyo inawaajiri watu wa kujitolea kuwambukizwa malaria kimakusudi kwa malipo ni ya kupotosha na si sahihi.”
Taasisi hiyo iliendelea kueleza kuwa Utafiti wowote wa KEMRI unaohusisha binadamu unafanywa chini ya uangalizi mkali wa kimaadili na udhibiti, kwa usalama wa mshiriki na ridhaa ya habari kama mahitaji ya msingi,"
Iliwashauri wananchi kutembelea chaneli zake rasmi za mawasiliano ili kupata taarifa sahihi, na kuthibitisha maudhui mitandaoni kabla ya kuyasambaza.
Na tuliangalia kwenye tovuti rasmi ya KEMRI na hatukupata taarifa kama hizo. Madai kuwa Kemri inatafuta watu wa kuwaambukiza Malaria kwa malipo ni uongo
28 juin 2026
Swahili (generic)
9 Mo