Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:00
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Michuano ya Chan2024 inaendelea na fainali inasakatwa hapo kesho Agosti 30 katika uwanja wa kimataifa wa Moi kule Kasarani nchini Kenya kati ya Madagascar na Morocco.
Kwa sasa mechi inayoendelea kutafuta nafasi ya tatu katika michuano hii ni Senegal na Sudan katika uwanja wa kimataifa wa Mandela nchini Uganda.
Wakati wa robo fainali timu zote wenyeji Kenya, Uganda na Tanzania ziliondelewa. Na wakati wa mechi kati ya Kenya na Madagascar, Harambee stars walipoteza na baadhi ya wakenya wakahisi refa aliwanyima nafasi ya kuingia nusu fainali.
Hili swala liliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, machapisho yakidai shirikisho la soka AfrikaCAF limeamuru kurudiwa kwa mechi kati ya Kenya na Mdagascar.
Chapisho la Facebook la Agosti 25 lilisoma
“Habari za hivi sasa: CHANN imekubali mechi ya marudiano Jumatano kati ya Kenya Vs Madagascar.” Mchapishaji alikuwa anarejelea Jumatano iliyopita na mechi hiyo haikuchezwa.
Mtumiaji mmoja alitoa maoni, "Ni ukweli kenya sasa Itapata fursa ya kuingia nusu fainali" Mwingine alisema. Mchapishaji mwingine kwenye Tiktok aliandika “ Mtumiaji mwingine wa Tiktok aliandika, "Kenya dhidi ya Mdagascar itakuwa na mechi ya marudiano tarehe 29 Agosti".
Napenda jinsi watu walivyo makini na taarifa za mitandaoni. Maana namuona hapa Duke Galilaya alijibu na kusema Kulingana na taarifa zilizopo, hakuna mechi rasmi ya marudiano iliyopangwa kufanyika kati ya Kenya na Madagascar.
Kwa sasa ni raia mmoja aliyewasilisha kesi kulalamikia hili, gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko akidai wasimamizi wa mechi walionyesha upendeleo na kukataa isivyo halali mabao mawili yaliyofungwa na Kenya. Hakuna mechi ya marudiano.
29 août 2025
Swahili (generic)
9 Mo