Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:53
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Sasa hivi watu wanazungumzia bahari ya Hormuz. Sasa video kwenye X imedai kuonesha meli ikiwaka moto baada ya kushambuliwa na makombora ya Iran kwenye Mlango huo. Ni taarifa inayokuja huku hali ikiwa tete katika Mashariki ya Kati.
Hata hivyo, vídeo inayosambaa, haina uhusiano wowote na hali ya sasa. Video ni tangu Julai 2024, baada ya moto kuzuka kwenye meli ya mizigo karibu na pwani ya India.
Tuanze kwa kuangalia chapisho kwenye X la Mei 4,
"VIDEO: MELI HUKO HORMUZ ILIPIGWA BOMU TU NA IRAN,".
Baadhi ya machapisho hayo yalidai kuwa video hiyo ilionyesha makombora ya Iran yakiigonga meli ya kivita ya Marekani kwenye mlango wa bahari, baada ya shambulio kuripotiwa na shirika la habari la Iran la Fars, ambalo Marekani ilikanusha.
Shirika la Fars pia lilisambaza video hii kwenye Telegram bila kusema mmliki wa meli, huku machapisho mengine yakidai kuwa meli hiyo ni ya Umoja wa Falme za Kiarabu, mengine yakidai ni meli kutoka Korea kusini.
Hata hivyo, chombo kwenye video si cha Marekani, Falme za Kiarabu au Korea Kusini -- na klipu hiyo haihusiani na vita vya Mashariki ya Kati.
Uchunguzi kupitia Reverse image search, umefichua kuwa gazeti la The Times of India lilichapisha picha zinazofanana kwenye Facebook na X mnamo Julai 19, 2024, likiripoti kwamba lilioyesha moto ndani ya meli ya mizigo kwenye pwani ya Goa, India.
Kituo hicho kilisema meli hiyo ilikuwa imebeba "bidhaa hatari za kimataifa za baharini". Walinzi wa Pwani ya India walichapisha picha za ziada za meli hiyo kwa akaunti yake rasmi ya X mnamo 2024.
09 mai 2026
Swahili (generic)
9 Mo