Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:59
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Tunaangazia uvumi unaozunguka madai ya kifo cha waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu.
Habari nyingine tumekutana nayo, ni ile ambayo imekuwa mitandaoni tangu Machi 12, kuhusu kifo cha Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.
Nakumbuka ilianza na video ya hotuba ya Netanyahu na watumiaji wengi wa mtandao walidhani wanaweza kuona hadi vidole sita. Uvumi huu ulichochewa zaidi na ukimya wa takriban saa 48 kutoka kwa Netanyahu.
Uchambuzi mbalimbali wa watu mitandaoni ulionesha wazi kuwa Netanyahu alikuwa amejeruhiwa au kufa, na mamlaka za Israeli zinasambaza video za uongo.
Ili kukomesha uvumi huo, Netanyahu alitoa video siku ya Jumapili akiwa kwenye mgahawa wa Jerusalem akinywa kahawa, na kuonesha wazi alikuwa na vidole vitano.
Video hiyo haikutuliza hali bali iliendeleza hisia zaidi, na watumiaji wakageukiwa Akili Mnemba ukipenda AI. Kwa mfano kwenye X, waliuliza Grok, ambayo pia ilidai kuwa vídeo ilikuwa imetengenezwa na AI.
Ndio maana wataalam wameonya kuwa AI na vigunduzi vyake lazima vitumike kwa tahadhari kwa kuwa sio za kutegemea kwa asilimia 100.
Kuthibitisha kuwa Netanyahu hajafa, Ijumaa ya Machi 20, Netanyahu ametoa video na hata kukanusha madai hayo. Pia alifanya tathmini ya hali ya usalama katika Kamandi Kuu na picha kuchapishwa.
Soma piaNipo hai: Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israeli
Pia Jumapili iliyopita, Netanyahu alitembelea eneo lililoshambuliwa na baadaye kuhutubia waandishi wa habari kuhusu Iran kurusha makombora ya masafa marefu. Hata Jumanne wiki hii ametoa hotuba. Msikilizaji Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel yuko hai, kinyume cha uvumi unaonea mtandaoni.
28 mars 2026
Swahili (generic)
9 Mo