Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Wiki hii tunakanusha madai kwamba Rais Trump wa Marekani ametoa wito wa kurejeshwa madarakani kwa rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila.
Kwenye mtandao wa TikTok, kuna chapisho lililosambazwa na watumiaji kadhaa likiambatana na picha za rais wa Marekani Donald Trump pamoja na sauti inayodai kuwa ametoa wito wa kurejeshwa madarakani kwa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila.
Hata hivyo, baada ya kufanyiwa uhakiki, imebainika kuwa taarifa hiyo si ya kweli na imetengenezwa kwa kutumia akili unde AI. Ingati tangu Juni 2026, machapisho kadhaa yamekuwa yakisambaa mitandaoni yakiwemo ya uongo kuhusu tafiti za maoni yakihusisha mashirika ya kimataifa pamoja na unabii unaotangaza kurejea madarakani kwa Joseph Kabila.
Baadhi pia wanadai kuwa muungano wa upinzani, unaojulikana kama C64, unaopinga marekebisho ya katiba nchini DRC, unaendeleza mikakati hiyo.
Sasa ni katika muktadha huu, ambapo tulianza mchakato wetu wa kuhakiki kwa kutafuta kauli za hivi karibuni za hadhara zilizotolewa na Rais wa MarekaniDonald Trump, ili kuona kama alimtaja Joseph Kabila, tukitumia maneno haya muhimu kwenye Google: "Donald Trump-Joseph Kabila-Kurejea mamlakani."
Matokeo hayakuonyesha chochote. Hakuna nakala za vyombo vya habari wala taarifa kutoka kwa chama cha Joseph Kabila za kukaribisha tangazo hili linalodaiwa kutolewa na Trump.
Kurejea madarakani kwa Joseph Kabila, kwa kuungwa mkono na Donald Trump, bado ni jambo la kufikirika tu. Tangu mwezi Mei 2016, kiongozi huyo wa zamani wa Kongo amekuwa chini ya vikwazo vya Marekani. Na tukawa tunatafakari, inakuwaje mtu aliye chini ya vikwazo vya Marekani akaungwa mkono na nchi hiyo hiyo?
Mbali na vikwazo vya Marekani; tangu mwaka wa 2025, rais wa zamani wa DRC amehukumiwa kifo na Mahakama Kuu ya Kijeshi ya Kongo kwa makosa ya kivita, ikiwemo ubakaji, mauaji, kutukuza uhalifu wa kivita, uhaini, kula njama, na kueneza propaganda za uhalifu wa kivita.
Tulikagua sauti ya maudhui tunayochunguza kwa kutumia Deepfake Total, zana ya kugundua sauti iliyotengenezwa kwa akili unde (AI). Ilionyesha uwezekano wa asilimia 100 kwamba ni *deepfake*.
Madai kwamba rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito wa Joseph Kabila kurejea madarakani kama rais wa DRC si ya kweli. Na sauti inayosikika katika video hiyo imetengenezwa kwa kutumia akili unde (AI).
24 juillet 2026
Swahili (generic)
9 Mo