Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Tunahakiki picha zilizobuniwa na AI zikidai mwanamuziki Fally Ipupa anafanya juhudi za kidiplomasia kukuza amani kati ya Rais Kagame na Macron.
Kwa miaka kadhaa, DRC na Rwanda zimekuwa na uhusiano wa mvutano kutokana na mzozo wa kiusalama haswa mashariki mwa DRC kutokana na kuwepo kwa makundi mengi yenye silaha na mapigano ya mara kwa mara.
Katika muktadha huu, mitandao ya kijamii imekuwa chanzo cha habari potofu. Kwa mfano picha tatu zimekuwa zimesambaa sana zikimwonyesha mwanamuziki Fally Ipupa akiwa pamoja na rais wa RwandaPaul Kagame na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Machapisho yanayoambatana na picha yanadai kuwa Fally amefanya juhudi za kidiplomasia ili kukuza amani akishirikiana na viongozi hao wawili.
Ni picha ambazo zimeibua maoni mbalimbali mitandaoni mmoja alitoa maoni akisema, "Fally ni raia wa dunia, na kwa kuwa muziki wa kisasa hauna mipaka, hakuna kinachomzuia kuwa na mashabiki kila mahali."
Watumiaji wengine kadhaa wa Facebook walizungumzia suala la AI: mmoja kaandika "Picha hizi zimetengenezwa kwa kutumia AI. Wizara ya Mawasiliano inapaswa kutekeleza wajibu wake kwa sababu upuuzi huu unazidi kuwa mkubwa."
Katika kuhakiki tunatapa chapisho la mtandaoni kutoka kwa chombo cha habari cha MBOTE.CD linalozungumzia likizo ya Fally Ipupa. Lilieleza kuwa Fally alikuwa kwenye likizo nchini Ugiriki.
Picha za awali, ambazo msanii Fally aliongezwa ndani yake, zilipigwa Jumanne, tarehe 2 Juni. Siku hiyo jijini Paris, Emmanuel na Brigitte Macron waliwakaribisha rais wa Rwanda na mkewe katika Ikulu ya Élysée, tukio lililowekwa kwenye akaunti ya Kagame.
Pia tumetumia zana za AI kuhakiki picha hii na tumepata kuna uwezekano wa asilimia 99 imeundwa na AI na hivyo kumaanisha picha hizi zikionyesha watatu hawa sio halisi.
Katika kuendelea kuhakiki, hakuna taarifa rasmi kuhusu mkutano kati ya Fally Ipupa, Paul Kagame na Emmanuel Macron. Kurasa rasmi za watatu hawa hazitaji mkutano wowote wa aina hiyo.
Na hakuna habari kama hiyo iliyochapishwa kwenye kurasa rasmi ya Facebook ya rais Paul Kagame, wala ya Emmanuel Macron au Fally Ipupa katika tarehe hizo.
Picha hizi zinazosambaa mtandaoni, zikimwonyesha Fally Ipupa akiwa na Rais Emmanuel Macron na mwenzake Paul Kagame, ni za kughushiwa kidijitali. Watatu hao hawajakutana kwa mazungumzo ya amani. Tumewasiliana na meneja wa Fally Ipupa lakini hadi kuenda hewani hawakuwa ametujibu.
08 août 2026
Swahili (generic)
9 Mo