Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:21
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Tunaangazia picha ya zamani ya ndege inayodaiwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii mashariki ya DR Congo kwamba imenunuliwa na waasi wa AFC- M23.
Picha ya ndege ambayo imeandikiwa "Air AFC-M23." Ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, haswa TikTok na Facebook, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Wanaoisambaza picha hii wanadai kuwa kundi la waasi wa AFC-M23 limeinunua ndege hiyo kwa ajili ya safari zao za kimataifa. Huu si ukweli. Ni picha ya Kampundi ya ndege ya shirika la Air France ambayo ilibadilishwa ilikudai kuwa ni ya waasi wa AFC- M23.
Kwa mengi zaidi usikose kusikiliza Makala ya Ukweli au Uongo Ijumaa saa 18:20 jioni saa za Afrika Mashariki.
Wakati tukiichunguza picha hii, kwanza tulitumia mbinu ya google AI ambapo google AI ilituambia kuwa na hapa ninanukuu "Picha inaonyesha ndege ya Air France Airbus A380, ambayo ni ndege kubwa zaidi ya abiria ya kibiashara kuwahi kutengenezwa."
Kutokana na majibu ya AI, tulitaka kupata maelezo zaidi, tuliendelea na uchunguzi zaidi wa picha hii, ambapo sasa tulitumia mbinu nyengine ya google reverse image search, tulipata picha nyingi tu zikiwa na madai hayo hayo kuwa ndege hiyo ni ya M23, picha ambazo zimekuwa zikisambaa tangu tarehe 7 Oktoba 2025.
Pia tulitumia maneno muhimu kwenye google kama vile "AFC/M23 yanunua ndege". Hapa hatukupata taarifa yoyote kuthibitisha kuwa waasi hao walikuwa wameinunua ndege wala hakuna chombo chochote cha habari cha kuaminika kutoka Kongo kilichapisha kuhusu hili.
Kati ya picha zote, ambazo tulichunguza kwa kutumia mbinu ya google reverse image search hatimaye tulipata picha ya kweli ambayo ilibadilishwa kudai AFC M23 ilikuwa imenunua ndege.
Picha iliyobadilishwa ni ya Airbus A380 inayomilikiwa na shirika la ndege la Ufaransa la Air France.
Picha ya ndege hiyo ya kampuni ya Air France ilikuwa imetumiwa katika taarifa kuhusu kusitishwa kwa safari za ndege nchini Ufaransa wakati wa mlipuko wa Uviko 19 au Corona.
Tukujuze tu kwamba katika picha inayodaiwa kuwa ya ndege mpya ya AFC- M23, nembo ya Air France ilibadilishwa na kuandikiwa Air AFC/M23, na rangi za bendera ya Ufaransa (bluu, nyekundu na nyeupe) kwenye bawa la ndege hiyo zilibadilishwa hadi kijani na nyeupe. Rangi ya nyasi kwenye barabara ya ndege ilisalia vilevile.
Tukujuze kwamba picha hii ni ya zamani na ni ya kampuni ya shirika la ndege la Ufaransa na sio uthibitisho kwamba waasi wa AFC- M23 wamenunua ndege.
16 janvier 2026
Swahili (generic)
9 Mo