Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:05
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Je uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Goma umefunguliwa? Uwanja huu umefungwa tangu kundi la M23 kudhibiti Goma Januari 2025.
Jijini Paris, wakati wa mkutano wa kuunga mkono amani katika eneo la Maziwa Makuu Oktoba 30, 2025, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, pamoja na mwenzake wa Kongo Félix Tshisekedi, walitangaza kufunguliwa tena kwa uwanja huo, tangazo ambalo halikupokelewa vizuri na kundi hilo.
Nakumbuka mnamo Februari 12, 2026, sehemu ya uwanja huo ilifunguliwa ikiashiria kutua kwa helikopta iliyombeba mkuu wa muda wa MONUSCO, Vivian van de Perre.
Hata hivyo, licha ya tukio hili, uwanja wa ndege bado umefungwa kwa safari za kila siku na misaada ya kibinadamu, licha ya wito wa mara kwa mara kutoka kwa mamlaka huko Kinshasa, Umoja wa Mataifa, na jumuiya ya kimataifa kwa ajili ya kufunguliwa tena.
Sasa katika muktadha huu, video kwenye Tiktok iliyochapishwa Machi 9, 2026, inaonesha ndege kwenye barabara ya ndege iliyozingirwa na ua, ikitangaza kufunguliwa upya kwa Uwanja wa Ndege wa Goma.
Katika sehemu ya maoni, watumiaji walionyesha mashaka au kupinga uhalisi wa tukio: Mmoja anasema "Unaota nini? Sahau hiyo rafiki zangu. Mimi ni jirani moja kwa moja; Sijui habari hizi", "Hii sio Goma," "Hebu ndugu zetu wanaoishi Goma watuhakikishie ikiwa habari hii ni ya kweli!", au hata "Ni Goma iliyo huko Kampala, Uganda."
Kuhakiki hili, kupitia mbinu ya Reverse Image Search, na tukagundua video inayoonyesha mazingira sawa, iliyochapishwa Februari 12, 2025 na mtumiaji wa Uganda anayeitwa "Bobshot" kwenye TikTok.
Kinyume na picha zinazozunguka, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Goma hauko katika eneo la mimea minene au msitu. Huwa umezungukwa na vitongoji vilivyo na miji mingi na watu wengi.
Vyanzo vya ndani ambavyo tumezungumza navyo, vimesema haabri hii ni ya uongo. Msikilizaji video hii inapotosha. Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Goma haujafunguliwa kama inavyodai video.
17 avril 2026
Swahili (generic)
9 Mo