Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:00
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Tutaanza kwa kuangalia picha za kupotosha kuwa ni za wahamiaji wa Marekani wanaowasili DRC.
Ni mwezi huu wa Aprili ambapo nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliwapokea wahamiaji kutoka Marekani kufuatia makubaliano ya nchi mbili yaliyohitimishwa mwezi huu.
Katika muktadha huu, machapisho kadhaa yamesambaa kwenye mitandao ya kijamii, yakidai kuonyesha picha za ujio huu nchini DRC. Baada ya kuchunguza, picha hizi zinatumika nje ya muktadha. Moja ni kutoka Mexico mwaka wa 2021 na Colombia mwaka wa 2025.
Tuangalie lilivyosema chapisho la Aprili 7, 2026 katika ukurasa wa Facebook wa Butembo News, na nanukuu
“Jiji la Kinshasa, litaanza kuwapokea wahamiaji haramu...Wakongo sasa watajifungua watoto wenye rangi tofauti siku zijazo."
Katika kuhakiki, tumetumia mbinu ya Reverse Image search, matokeo yametupelekea katika nakala iliyochapishwa mtandaoni kwenye Tribune de Genève, Agosti 31, 2021, iliriyopoti kuhusu kundi la wahamiaji kutoka Marekani Kusini ambao walizuiliwa na Walinzi wa Kitaifa wa Mexico.
Tulifanya vivyo hivyo kwenye picha ya pili, matokeo yalitupeleka kwenye nakala ya shirika la habari la Reuter, ya Januari 28, 2025. Maelezo yanasoma “Ndege ya Jeshi la Wanahewa la Colombia ilitua Bogota ikiwa na raia 110 waliofukuzwa nchini Marekani.”
Matokeo mengine yalitupeleka kwenye nakala kutoka Radio-Canada, iliyoandika kuhusu tukio la kufukuzwa mnamo Januari 28, 2025.
Ndio ni kweli kwamba DRC ilianza kutekeleza mfumo huu wa kuwapokea wahamiaji baada ya kusaini mkataba huo na Marekani, lakini kinyume cha machapisho, picha hizi sio thibitisho la kuwasili kwa wahamiaji nchini DRC.
Aprili 17, 2026, Wizara ya Mawasiliano na Vyombo vya Habari ya DRC ilisema: “Serikali inautaarifu umma kuhusu kuwasili Kinshasa kwa wahamiaji wa kwanza chini ya mpango wa mapokezi wa muda wa raia kutoka nchi zinazoendelea.”
Katika uchunguzi zaidi, hakuna chombo cha habari cha kuaminika kilichochapisha picha hizi, zinazosambazwa nje ya muktadha.
Moja ya picha ni kutoka Mexico (2021) na nyingine kutoka Colombia (2025). Matumizi ya picha za zamani kuonesha matukio ya sasa, ni mbinu inayotumika kusambaza taarifa potofu.
24 avril 2026
Swahili (generic)
9 Mo