Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:18
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Habari moja tutaangazia ni chapisho nchini DRC linalodai wakufunzi wa jeshi la Marekani tayari wako nchini Kongo kutoa mafunzo kwa vitengo maalum vya FARDC.
Chapisho la tarehe Agosti mosi mwaka huu kwenye mtandao wa X nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), linadai kuwa wakufunzi wa jeshi la Marekani tayari wako nchini Kongo kutoa mafunzo kwa vitengo maalum vya wanajeshi wa Kongo (FARDC).
Kule mashariki mwa DRC, maeneo kadhaa kwa muda sasa yameshuhudia ukosefu wa usalama na mchakato wa amani chini ya usimamizi wa Marekani ulisababisha kusainiwa kwa makubaliano ya amani kati ya Rwanda na DRC Juni 27, 2025, kule Washington.
Lengo la mipango hii yote ni kutafuta suluhu kwa mzozo huo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 30 katika eneo mashariki mwa DRC, na kufikia amani ya kudumu.
Hata hivyo, kwa kutumia Reverse Image Search kwenye google, picha hii ilipigwa wakati wa mafunzo ya kijeshi ya pamoja kati ya wakufunzi wa Marekani na kikosi maalum cha Ivory Coast wakati wa Zoezi la Flintlock, ni zoezi la kila mwaka linaloongozwa na Marekani kwa ushirikiano na nchi za Kiafrika.
Pia tulitafuta maneno muhimu yanayoambatana na picha kama vile, kutumwa kwa wanajeshi, Wamarekani, FARDC, na tulipata habari zilizoripotiwa ni kuhusu ushirikiano wa awali wa wakufunzi wa jeshi la Marekani kuwafunza wenzao wa Kongo, kati ya mwaka 2010 na 2020.
Kisha tukaangalia tovuti za Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Ubalozi wa Marekani nchini DRC na Wizara ya Ulinzi nchini DRC, na hatukupata taarifa zozote zilizochapishwa zikithibitisha kutumwa kwa wakufunzi wa Marekani nchini DRC kutoa mafunzo kwa vitengo maalum vya FARDC.
Picha asili ni kutoka kwa mazoezi ya Flintlock ya 2023 nchini Ivory Coast, na ilichukuliwa na Ashlind Moir, kutoka kitengo cha Operesheni maalum ya Marekani kwa Afrika ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayoitwa Flintlock kati ya wanajeshi wa Marekani na vikosi maalum vya Ivory Coast.
Picha si ya mafunzo kwa jeshi la FARDC nchini DRC, bali inatoka Côte d'Ivoire na ni ya 2023.
16 août 2025
Swahili (generic)
9 Mo