Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:57
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Tunaangalia picha za kiongozi mkuu wa Iran aliyefunikwa kwenye vifusi ambayo imeundwa kupitia AI.
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliuawa katika mashambulio ya pamoja ya Marekani na Israel yaliyoanza Februari 28, 2026, lakini picha zinazodaiwa kuonyesha maiti yake iliyofunikwa kwenye vifusi zimeenea kwenye mitandao ya kijamii.
Picha hizi ni sehemu ya kuongezeka kwa taarifa potofu mtandaoni kufuatia kifo cha kiongozi huyo wa muda mrefu wa Iran, na kwa kuzitazama kwa makini kwa kutumia zana za utambuzi, zina uwezekano wa kuundwa kwa AI.
Chapisho kwenye Facebook la Machi mosi, 2026, linasema
Vyombo vya habari vya kimataifa vilifichua picha ya mwili wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ambaye aliuawa katika shambulio la Marekani na mshirika wake Israel siku ya Jumamosi.
Picha inayoonekana kumuonyesha Khamenei akiwa amekufa amezingirwa na vifusi, ilisambazwa juu ya video kutoka kwenye shirika la habari la Al Jazeera kuhusu kuuawa kwa Ayatollah.
Picha sawia na hiyo inayoonekana kuwaonyesha waokoaji wakiondoa kifusi kutoka kwenye mwili wa Khamenei pia ilishirikiwa siku hiyo hiyo kwenye X, ikisema: "Iran yatoa picha ya mwili wa Khamenei chini ya vifusi."
Picha hizo pia zilishirikiwa kwenye YouTube na X katika lugha nyingi, walakini, hakuna picha rasmi za mwili wa Khamenei ambazo zimetolewa, na picha zinazosambaa mtandaoni zimeripotiwa kuundwa kupitia AI.
Ukiangalia kwa makini katika picha iliyosambazwa kwenye Facebook, utaona picha hiyo ina lebo ya "Meta AI".
Wafanyakazi wa uokoaji katika picha iliyotengenezwa na AI pia wanatofautiana na wale wanaoonekana kwenye picha za juhudi za uokoaji zilizochukuliwa na mashirika ya habari kama vile AFP.
Kuna adhabu kali za kisheria zimetolewa haswa na serikali ya UAE, ukipatikana na hatia ya kueneza habari potofu, unaweza kufungwa jela au faini isiyopungua elfu 200 pesa ya UAE ambayo si chini ya dola elfu 54.
07 mars 2026
Swahili (generic)
9 Mo