Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Picha inayodai wanajeshi wa Kenya wametumwa hivi maajuzi kule Uvira Mashariki mwa DRC japo picha hii ni ya mwaka 2022.
Kuna picha imekuwa ikisambaa mitandaoni wanavyosema haswa katika makundi kadhaa ya Wahtsapp ikionesha malori kadhaa ya kivita yenye bendera za Kenya.
Maelezo yanadai picha inaonesha kuwasili kwa wanajeshi wa Kenya huko Uvira, mji wa jimbo la Kivu Kusini mashariki mwa DRC, kwa lengo la kuimarisha jeshi la Kongo dhidi ya waasi wa M23.
Baada ya kuthibitishwa, habari hii imepatikana kuwa ya uwongo; picha hiyo ni ya kutoka mwezi Novemba mwaka 2022 na ilichukuliwa katika jiji la Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.
Katika kuhakiki tumepata kuwa picha hii imechukuliwa nje ya muktadha. Taarifa hizo zinasamabzwa wakati huu kukiwa na wasiwasi katika mji wa Uvira, ambao pia unakabiliwa na vitisho vya waasi wa M23.
Na tulipotafuta kwenye Google, tukitumia maneno muhimu kama vile, Uvira, Wanajeshi wa Kenya, hatukupata matokeo yenye tija kuhusu hili. Pia hakuna vyombo vya habari, wala machapisho yaliyothibitisha kuwasili kwa wanajeshi wa Kenya katika eneo hilo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Halkadhalika, tulipotafuta picha hii kupiti Reverse Image Search tukitumia picha inayoenezwa, utafutaji ulituletea nakala chache za vyombo vya habari zinazoitaja pamoja na machapisho ya video.
Kiuhalisia, picha hii ni ya kutoka Novemba, mwaka 2022, wakati wanajeshi wa Kenya walipowasili katika mji wa Goma, wakiwa sehemu ya kikosi cha pamoja cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, ili kupambana na waasi wa M23 waliokataa kuondoka katika maeneo waliyokuwa wakimiliki wakati huo.
Pia tumeangalia katika mtandao wa X na tukapata chapisho la mwaka 2022 likiwa na vídeo maandishi juu yake yakisema
“Mapigano ya #RDC #FARDC-#M23, vifaa vya kivita vya wanajeshi wa #Kenya viliwasili Goma Jumatatu hii, Novemba 28. Kamanda wa kikosi cha #EAC anasema kuwa wanajeshi wake wanajituma ardhini huko #Nyiragongo kupambana na waasi.
Ndicho kipindi unachosikiliza hewani katika Idhaa hii ya RFI Kiswahili, sote tunajitahidi kueneza habari za ukweli, ambazo hazipotoshi haswa katika mitandao ya kijamii.
29 novembre 2025
Swahili (generic)
9 Mo