Podcasts
Enjeux de société
Erdogan hints at larger nuclear partnership with Russia, unsettling Turkey's allies
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Tangu Jumamosi Oktoba 11 mwaka huu, kumekuwepo na video kwenye mitandao ya kijamii haswa kwenye X ikidai kuonesha mapinduzi kule Kinshasa nchini DRC na kutoweka kwa rais Félix Tshisekedi. Walakini, huu ni uongo video hii ni ya Antananarivo, Madagaska.
Chapisho linasoma
"Kinshasa imeanguka! Rais hapatikani popote! Wazalendo chini ya uongozi wa Bitakwira wameanzisha mapinduzi!"
Ili kuhakiki, tumeanza kwa kufanya utafiti kwenye google, kwa kutumia picha ya skrini ya video, na uchanganuzi wetu ulibaini kuwa video hiyo ilirekodiwa huko Antananarivo, Madagaska.
Video hiyo hiyo pia ilichapishwa kwenye Facebook na hapa inasema
"Serikali ya Madagaska imeanguka. Polisi walijiunga na waandamanaji, na rais akakimbia nchi."
Halkadhalika kwenye mtandao wa X tulipata pia video ya Oktoba 11 ikiwa na maoni sawa na hayo kwamba
"Wanajeshi nchini Madagascar wamekataa amri ya kuwapiga risasi waandamanaji!! Uongozi"
Kwa kutumia mbinu ya Geolocation, hii inatumika kutambua sehemu video au picha imechukuliwa, tuligundua kuwa alama za "Pharmacie de l'avenue" na "MVola" zinaonekana kwenye majengo huko Antananarivo, Madagaska na hivyo kuthibitisha kwamba video haionyeshi Kinshasa, DRC.
Uchunguzi zaidi unaonesha hakuna vyombo vya habari vya Kongo au vya kimataifa vilivyoripoti mapinduzi yoyote ya Kinshasa na makala iliyochapishwa Jumapili ya Oktoba 12, kwenye tovuti rasmi ya Urais wa DRC inabainisha kuwa Félix Tshisekedi alikuwa Ubelgiji, ambako alikuwa amezungumza na wakongomani wanaoishi huko.
.
24 octobre 2025
Swahili (generic)
9 Mo