Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:59
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Kuna picha inasambaa mitandaoni ikidai vikosi vya Ukraine vimemkamata rais wa Belarus Alexander Lukashenko. Ni madai yanayokuja baada ya mwezi Juni Ukraine kuishtumu Belarus dhidi ya kuisaidia Urusi katika mashambulizi ya ndege zisiso na rubani.
Hata hivyo, hakuna ripoti rasmi zinazoonyesha kuwa Lukashenko amekamatwa na picha hii imegunduliwa kutenegenzwa na AI. Sehemu ya chapisho la Facebook la tarehe 6 Julai 2026 inasema, "Wapiganaji wa Ukraine walidai kumkamata Lukashenko wakiwa katika himaya ya Belarus,".
Chapisho pia linajumuisha picha inayoonekana kumwonyesha Lukashenko akishikiliwa na askari wawili waliovalia sare zenye nembo ya bendera ya Ukraine.
Kwa miezi kadhaa, Ukraine imekuwa ikiionya Belarus dhidi ya kuhusika zaidi katika vita hivyo. Hata hivyo Lukashenko amekanusha kuwepo kwa mipango ya kuhusika moja kwa moja katika vita hivyo.
Lakini hata hivyo hakuna ripoti rasmi zinazoonyesha kuwa Lukashenko amekamatwa, na picha hiyo ilitengenezwa kwa kutumia akili unde (AI). Uchunguzi wa kina wa picha hiyo unaonyesha nembo ya Gemini katika kona ya chini upande wa kulia. Hii ni zana ya Google.
Pia inaonyesha kasoro ambazo mara nyingi huonekana katika maudhui yaliyotengenezwa AI, ikiwa ni pamoja na pingu zinazoonekana kana kwamba zinaning'inia hewani na nembo tofauti kwenye helmeti. Sare nyingine pia zina nembo ya kijeshi ya Huduma ya Usalama ya Ukraine (SBU), huku nyingine zikiwa hazina nembo hiyo.
Uchambuzi uliofanywa kwa kutumia zana ya Google ya SynthID umethibitsisha kuwa picha umeundwa kupitia AI. Lukashenko pia alihudhuria hafla rasmi siku hiyo hiyo ya madai kuenea na hata wiki kadhaa baada ya chapisho hilo la uongo kusambaa.
Pia alikutana na afisa wa Urusi, Igor Shchegolev, mnamo Julai 27. Msikilizaji hakuna ripoti rasmi zinazoonyesha kuwa Lukashenko amezuiliwa na vikosi vya Ukraine. Picha imeundwa kupitia AI.
31 juillet 2026
Swahili (generic)
9 Mo