Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:00
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Tangu Novemba, 3, 2025, ukurasa wa facebook kwa jina, Swahili Fasil kwa maana ya kiswahili kinachoeleweka na kila mtu, ukurasa huu una wafuasi zaidi ya elfu 85, ulichapisha habari ya kupotosha inayodai kampuni ya maji ya Yme Jibu, ilisambaza maji chafu yenye rangi ya njano kwa wakazi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Yme Jibu ni kampuni ya kibinafsi inayoihudumu kule Goma, DRC, ambayo hutoa upatikanaji endelevu wa maji safi ya kunywa. Kampuni hii inayasafisha maji kutoka Ziwa Kivu kabla ya kuyasamabza kwa wakaazi, wafanyabiashara, na taasisi mbalimbali.
Ripoti ya mwaka 2021, inasema kampuni ya Yme Jibu ilihudumia takriban watu laki themanini na tatu, ikilenga kuongeza idadi hii, ambapo uwepo wake wa kuwa chanzo cha maji cha uhakika, umeboresha kwa kiasi kikubwa afya na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika maeneo inayohudumu.
Chapisho hilo lilipata maoni kadhaa na kusambazwa kwa makundi mbalimbali, nisome moja ya maoni yake Aboubakar Munyamariba.
“Wanapaswa kujaribu zaidi, maji ni machafu sana. Kwa hakika, mvua inaponyesha, maji ya mvua huwa safi ikilinganishwa na yale wanayotoa.”
Chapisho hili pia lilitumwa kwetu na mwenzetu wa kutoka kule Goma Benjamin Kasembe.
Katika kuhakiki, tulifanya mahojiano na Jacque KAHORA, mkuu wa shirika la Yme Jibu ambaye alipuuzilia mbali shutuma hizo akisema shirika lake linasambaza maji safi kwa wakaazi wa Goma.
Kauli yake ilithibitishwa mwandishi wetu wa Goma Benjamin Kasembe baada ya uchungizi katika maeneo husika.
Kwa mujibu wa ukurasa wa Facebook wa Swahili facile, walipokea habari hizo kutoka kwa wakazi wa eneo hilo, lakini baadaye walitembelea maeneo husika na kupata sivyo walivyojulishwa.
Na mnamo Novemba 5, ukurasa huo ulikanusha habari hiyo na kuandika ile sahihi baada ya mawasiliano kutoka kwa kampuni hiyo, iliyosema kuwa habari hii imetungwa.
15 novembre 2025
Swahili (generic)
9 Mo