Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:57
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Ushindani mkubwa zaidi wa ligi ya mabingwa mwaka 2026 barani Ulaya ulifikia tamati baada ya PSG kushinda kwa penalti 4-3, dhidi ya Arsenal mnamo Mei 30, 2026.
Ushindani mkubwa zaidi wa ligi ya mabingwa mwaka 2026 barani Ulaya ulifikia tamati baada ya PSG kushinda kwa penalti 4-3, dhidi ya Arsenal mnamo Mei 30, 2026.
Chapisho la tarehe 7 Juni lilidai UEFA imetangaza kufutwa kwa matokeo ya fainali hiyo, na kuamuru PSG kurudisha kombe hilo, na huku tarehe mpya ya mechi ya marudiano ikiratibiwa.
Chapisho kama hilo lilichapishwa na akaunti nyingine ya facebook ikisema
“Habari za hivi sasa! Uefa imeipokonya PSG taji la Ligi ya Mabingwa na kuwapa Arsenal."
Madai yaleyale yalichapishwa kwenye Youtube na madai ya ziada kuwa Fifa imechukua hatua na kumsimamisha kazi kocha wa PSG.
Sasa, Je PSG imevuliwa ubingwa? Uvumi huo ni wa uongo na unatokana na habari ghushi zinazosambaa mitandaoni kufuatia ushindi wao.
PSG ndio Mabingwa rasmi, baada ya kutwaa mataji mfululizo ya Ligi ya Mabingwa kwa kuishinda Arsenal kwa mikwaju ya penalti mjini Budapest.
Huenda mkanganyiko huu ulitokana na kanuni tofauti, ya kawaida ambapo UEFA huruhusu timu kuhifadhi mfano wa ubora wa juu kwenye kabati lao huku shirikisho hilo likihifadhi kombe halisi.
Chini ya Kifungu cha 1 kuhusu umiliki, cha Kanuni za Kombe la Dunia la FIFA, timu inayoshinda itaruhusiwa kunyanyua kombe halisi uwanjani wakati wa hafla rasmi ya utoaji wa zawadi, kisha litarejeshwa mara moja kwa FIFA na kuwekwa kwenye Jumba la Makumbusho la FIFA huko Zurich.
13 juin 2026
Swahili (generic)
9 Mo