Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:00
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Moja ya habari tunayoangazia ni machapisho ya mitandoani yanayodai mji wa Uvira unajitawala na umeunda serikali yake, madai ambayo naibu meya ameyakanusha.
Shughuli Mjini Uvira nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, zilirejea kawaida Jumatatu baada ya kushuhudiwa kwa maandamano yaliyopangwa na mashirika ya kiraia na wapiganaji Wazalendo.
Maandamano haya yalikuwa kupinga uteuzi wa jenerali Olivier Gasita kama mkuu wa operesheni za kijeshi katika eneo hilo, akishutumiwa kwa kuwa na uhusiano wa karibu na waasi wa AFC/M23 kwa kuwa ametokea jamii ya Banyamulenge.
Kwa mujibu wa msemaji wa Operesheni ya Sokola 2, Luteni wa Pili Reagan Mbuyi Kalonji, fujo hizo zilisababisha kifo cha mtoto wa miaka 12 na wengine tisa wakiwemo askari 4 wa FARDC na raia 5.
Kutokana na hali kule Uvira, tangu Jumapili ya Septemba 7, kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kiongozi wa wapiganaji wa #Wazalendo, Amuri Yakutumba, ametangaza maeneo ya #Uvira, #fizi na #Mwenga kuwa yataanza kujisimamia.
Katika chapisho hili, kuna orodha ya majina na nyadhifa za serikali hiyo inayodaiwa kuwa ya Uvira zikiwemo; Rais, Waziri Mkuu, Mkuu wa Majeshi, Naibu, Kamanda wa Operesheni na Mkuu wa Mkoa. Chapisho pia lina bendera iliyo na rangi karibu sawa na ile ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hata hivyo, rangi zimebadilishwa.
Kutoka juu, bendera ina rangi ya bluu, katikati ni njano, chini ina rangi nyekundu wakati katikati kuna miduara miwili ya bluu na nyeupe na maandishi meusi ya jamhuri ya Uvira.
Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ina rangi tatu: bluu isiyokolea, nyekundu na njano. Sasa swali ni je, mkoa wa Uvira umeunda serikali yake?
Katika mahojiano ya kipekee na RFI Kiswahili wiki hii, Meya wa Uvira, Kivu Kusini mashariki mwa DRC, Kifara Kapenda alikanusha taarifa hizo akisema hazina ukweli wowote na ni uzushi kwenye mtandao.
12 septembre 2025
Swahili (generic)
9 Mo