Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:06
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Moja ya habari tunaangazia wiki hii, ni video inayodai wanajeshi wa Chad wako nchini DRC kupambana na M23.
Hali ya usalama kule Mashariki mwa DRC, ni ya kusuasua na kufikia Desemba 2025, ghasia ziliongezeka, na kusababisha mgogoro wa kibinadamu, zaidi ya watu milioni 28 wakiathirika hii ikiwa idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa nchini humo pamoja na mzozo wa kidiplomasia.
Sasa video ya sekunde 20 iliyoshirikiwa kwenye X mnamo tarehe 17 Desemba 2025 ina madai haya ninayoyanukuu
"Vikosi maalum vya Chad viliingilia kati kukabiliana na waasi wa AFC-M23, baada ya M23 kushinda kikosi kikubwa cha pamoja: Kikosi kilichorejelewa hapa ni FARDC-FDLR-Wazalendo-Mai-Mai-mamluki wa Romania-majeshi ya Burundi-SADC na Afrika Kusini. Chapisho linamalizia kwa kuuliza: Je, Chad itaweza kuwazuia?"
Video hii ilitazamwa na zaidi ya watu elfu 48 na wacha nisome moja ya maoni kwenye video hii"Ninapendekeza kwa Chad kusoma ujumbe huu kabla ya kuivamia nchi. Labda wanapaswa kujiuliza wamejiingiza katika nini."
Je video hii ni ya ukweli? Tulichukua picha ya skrini kutoka kwenye video, kisha kuanza kuihakiki kwenye google lens na majibu tuliyopata “Picha inaonyesha wanajeshi wakiwa na magari ya MRAP, magari ambayo yametengenezwa kutoka Nigeria na hutumiwa na jeshi la Chad kwa operesheni zao.
Uthibitishaji zaidi unasema magari haya ya "Proforce MRAPs yalionyeshwa wakati wa kusherehekea ya Sikukuu ya 62 ya Uhuru wa Chad. Magari hayo yameundwa kustahimili shambulio la kuvizia na mashambulizi ya vilipuzi."
Uchunguzi zaidi unatupeleka kwenye video iliyochapishwa kwenye Facebook na Ukurasa unaoitwa "Proforce", wenye maelezo kuwa muungano wa kimataifa unaojumuisha makampuni yanayoongoza katika utaalam wa usalama wa kijeshi na raia.
Video hii ya Agosti 11, mwaka 2022 ina kichwa "Angalia Proforce MRAPs kwenye maonyesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya 62 ya Uhuru wa Jamhuri ya Chad.
Katika utafutaji kwenye google iwapo majeshi ya Chad yametumwa DRC Desemba 2025, hakuna ripoti kutoka kwa vyombo vya habari vya ndani au vya kimataifa, matokeo ya utafutaji yananukuu makala kutoka 1998, wanajeshi hao walipoingia Kongo kupigana pamoja na vikosi vilivyokuwa vinamuunga mkono Rais wa zamani Laurent Kabila dhidi ya waasi."
Video hii sio ya sasa hivi ni ya Agosti mwaka 2022 nchini Cahd wakati wa awamu ya 62 ya siku ya uhuru na wala sio ya vikosi vya Chad nchini DRC hivi maajuzi.
03 janvier 2026
Swahili (generic)
9 Mo