Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:00
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Tunaangalia video inayodai rais Macron akikosoa India katika ziara yake nchini humo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitembelea India mwezi huu, na sasa kuna video ghushi inamuonesha Macron akikosoa Jeshi la Wanahewa la India. Mapitio ya hotuba yake ya asili iligundua kuwa hakutoa matamshi yaliyoonyeshwa kwenye video, ambayo sauti yake inaonekana kubuniwa kwa kutumia AI.
Chapisho kwenye X la Februari 18 linasoma
“Habari ya sasa hivi: Emannuel Macron afichua siri kwenye Mkutano wa India wa AI," Inaangazia video ya Macron akimwambia Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwamba Ufaransa "haiwezi kuwa mshirika kamili wa ulinzi na India".
Ziara ya Macron ya siku tatu India, ilifuatia uthibitisho wa New Delhi kwamba inakusudia kuagiza ndege za Dassault Rafale, pamoja na kusainiwa kwa makubaliano ya kihistoria ya biashara huria kati ya India na Umoja wa Ulaya.
Hata hivyo katika kuhakiki, klipu inaonesha matamshi yaliyoonyeshwa kwenye video hiyo ni ya kubuni.
Kwa kutumia mbinu ya Reverse image search, kwenye video bandia, uhakiki ulitupeleka hadi video ya tukio lile lile iliyooneshwa katika chaneli ya Youtube ya rais wa Ufaransa mnamo Februari 17.
Video inamuonesha Macron akizungumza Kifaransa muda huo wote. Video inayozunguka inaonekana kutolewa katika video hiyo katika dakika ya 27:52. Ofisi ya rais wa Ufaransa ilichapisha hotuba ya Macron, akitoa matamshi yake kwa Kifaransa na si yale yaliyosikika kwenye video inayosambazwa.
Pia ofisi ya Waziri Mkuu wa India ilipeperusha mazungumzo hayo moja kwa moja kwenye chaneli yake rasmi ya YouTube siku hiyo hiyo, ambayo iliyataja matamshi ya rais wa Ufaransa kwa Kihindi.
India na Ufaransa zilichapisha taarifa rasmi ya pamoja Februari 17, na hakuna ukosoaji dhidi ya jeshi la India. Uchambuzi wa sauti ya video unaonyesha uwezekano wa asilimia 98.8 kuwa sauti hiyo imeundwa na AI.
Pia kwa kutumia mbinu ya InVID-WeVerify, inaonyesha baadhi ya sehemu za hotuba ni sauti ya AI.
28 février 2026
Swahili (generic)
9 Mo