Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:55
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Kwenye mtandao wa X habari inapotosha ikisema mkutano wa nchi za maziwa makuu huko Ufaransa ulikuwa wa kusema kuwa Rwanda inatekeleza mauaji.
Tarehe 30 Oktoba, 2025, Ufaransa kwa ushirikiano na Togo mpatanishi wa Umoja wa Afrika kwa Maziwa Makuu, waliongoza mkutano jijini Paris ili kuunga mkono amani na ustawi katika eneo hilo haswa kuhusu mgogoro wa muda mrefu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
Ni mkutano uliotarajiwa kuhudhuriwa na wakuu kadhaa wa nchi za Afrika, hata hivyo, ni viongozi wawili tu wa Afrika waliohudhuria, Rais wa DRC Felix Tshisekedi na mwenzake wa Togo, Faure Gnassingbe.
Mataifa mengine mengi yaliwakilishwa na mawaziri wao wa mambo ya nje au wajumbe maalum, ikiwa ni pamoja na Rwanda, iliyowakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje Olivier Nduhungirehe.
Katika mkutano huo, Rais wa UfaransaEmmanuel Macron alitangaza uhitaji wa euro bilioni 1.5, msaada wa kimataifa kushughulikia dharura ya kibinadamu nchini DRC, huku akiahidi kupeleka chakula na dawa, na kuanzisha njia salama za misaada.
Tangu kipindi hicho, picha imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii haswa kwenye X ikidai kuonyesha bango lililoandikwa na nalinukuu
"RWANDA INAUA Mkutano wa Paris kuhusu Mgogoro wa Kibinadamu, Maziwa Makuu: "
Akaunti nyingine ya X mnamo October 31 iliandika “Ukweli mtupu #RWANDA INAUA. Picha hiyo pia ilitumika kwenye video katika Youtube
Je, picha hii ni ya kweli? Tulianza kwa kutumia google kwa kuweka picha hiyo kwenye google lens na tukapata picha hiyo imehaririwa na kuongeza maandishi kuwa “Rwanda Inaua”
Tulikagua zaidi ikiwa picha ilikuwa imeshirikiwa na chanzo chochote cha kuaminika. News.cd, Ukurasa rasmi wa facebook unaochapisha habari za kisiasa, usalama na kiuchumi kutoka DRC, siku hiyo hiyo ilichapisha picha ambayo haina maandishi "RWANDA INAUA" kwa herufi kubwa.
Naye msemaji wa rais Tshisekedi Tina Salama, kwenye mtandao wake wa X alichapisha picha ambayo si ya kupotosha kuwa Rwanda inatekeleza mauaji.
Pia tuliangalia kwenye akaunti ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe, ambaye alihudhuria mkutano huo, chapisho lake liliambatana na lile kutoka kwa wizara anayoiongoza kwenye akaunti yake ya X. Si kweli, mkutano huo haukuwa kuhusu "Rwanda Inaua" kama bango linavyodai lakini miongoni mwa masuala muhimu ilikuwa ni usaidizi wa kimataifa kushughulikia dharura ya kibinadamu nchini DRC.
07 novembre 2025
Swahili (generic)
9 Mo