Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:57
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Huku maelfu ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini wakikimbia, machapisho ya mitandao ya kijamii yalidai kwamba Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliwaambia raia wake warudi nyumbani kwa miguu.
Lakini hii ni uongo; madai hayo yalitokana na ukurasa wa Facebook wa kejeli na ni picha ya rais Mnangagwa akihuutbu katika mkutano wa kilele wa mwaka 2025 nchini Kenya.
Chapisho kwenye X la Juni 16 linasoma, "Rais wa Zimbabwe Anasema Watu Wake Watarudi Nyumbani Kama Walivyotembea hadi Afrika Kusini; Hana Bajeti ya Kuwasafirisha Bure Kabla ya Juni 30,"
Chapisho hilo likiwa limeshirikiwa zaidi ya mara 1,600, lina nembo ya Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC). Mnangagwa akiwa katika picha kwenye jukwaa katika ukumbi wa Kimataifa cha Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi.
Madai haya yameibuka huku kukiwa na ongezeko la mvutano dhidi ya wageni na wito wa baadhi ya makundi yanayoongozwa na raia kutaka wahamiaji wasio na vibali kuondoka nchini humo, jambo ambalo limeongeza wasiwasi kufuatia wiki kadhaa za machafuko.
Ndio maandamano ya kupinga uwepo wa raia wa kigeni nchini Afrika Kusini yalifanyika Juni 30, siku iliyokadiriwa kuwa makataa ya wageni kuwa nchini humo, lakini madai dhidi ya Rais Mnangagwa si ya kweli.
Tunapotumia mbinu ya Reverse Image Search, picha ya skrini ya KBC imebadilishwa kutoka kwa picha za Mnangagwa akizungumza katika mkutano wa 24 wa wakuu wa COMESA nchini Kenya mnamo 2025.
Video ya dakika saba iliyochapishwa na KBC mnamo Oktoba 9, 2025, kwenye YouTube inaonyesha Mnangagwa akihutubia mkutano huo. Fonti na ukubwa wa maandishi yametofautiana.
Mnangagwa hakurejelea Wazimbabwe wanaorejea nyumbani. Taarifa hii ilitokana na ukurasa wa Facebook wenye maudhui ya kejeli. Chapisho hilo linamalizia kwamba "nakala hiyo ni kejeli na imekusudiwa kwa ucheshi tu".
Si kweli kuwa rais wa ZimbabweEmmerson Mnangagwa amewataka raia kurudi nyumbani kwa miguu kutoka Afrika kusini.
04 juillet 2026
Swahili (generic)
9 Mo