Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Tunahakiki picha nne zilizowekwa pamoja zikienezwa mitandaoni haswa kwenye Facebook tangu tarehe 7 Agosti, ikiambatana na madai yafuatayo na nanukuu: “Makao Makuu ya Jeshi la FARDC yamesimamisha operesheni ya mashambulizi katika pande zote. Wanasubiri kinachokuja Bujumbura; #Burundi ndiyo kituo kilichochaguliwa na Wamarekani kwa ajili ya makabiliano ya moja kwa moja.”
Chapisho linaendelea kusema “Sasa, kuwasili kwa wapiganaji wa Jihad ni kukomesha umwagaji huu wa damu, huku mashambulizi yetu yakizidi kushika kasi. Wanyarwanda wanadhani wameshinda vita hivi, wakisaidiwa na wapiga-propaganda wa Kikongo wanaounga mkono Rwanda na kusambaza habari za uongo.”
Picha hii inasambaa nchini DRC kama ushahidi wa kuwasili kwa wanajeshi na vifaa vya kijeshi vya Marekani nchini Burundi, ambavyo baadaye vitapelekwa mashariki mwa DRC kupambana na Rwanda na China.
Picha ina vichwa tofauti. Kwenye Facebook kichwa kinasema “#Bujumbura, Vikosi vya Marekani kutua DRC; Rwanda yaingiwa na hofu.” Kwenye YouTube kichwa kilisoma "Dharura: Marekani yatuma ujumbe mzito kwa Rwanda huku ndege ya kijeshi ya Marekani ikitua Burundi."
Sasa baada ya kuhakiki, picha hizi hazina uhusiano wowote na Afrika. Picha ya kwanza ilitokana na mahojiano maalum na Seneta Olivier Cigolotti—mtaalamu wa migogoro ya kijeshi na Jeshi la Ufaransa. Katika mahojiano na kituo cha habari cha Zoom dici, anaelezea wasiwasi wake kuhusu mustakabali wa amani barani Ulaya. Mahojiano yaliyochapishwa Novemba 2025.
Picha ya pili, inatoka kwenye makala iliyochapishwa mtandaoni mnamo Aprili 2024, ikizungumzia matembezi ya 'Carentan Liberty March' yaliyopangwa kufanyika tarehe 8 Juni 2024, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 80 tangu kutua kwa majeshi huko Normandy, Ufaransa.
Picha ya tatu, inayodaiwa kuonyesha ndege ya Marekani ikitua, tuliipata kwenye Pik roll. Hiki ni chanzo cha maudhui ambapo unaweza kupata picha, nyaraka na vitu vingine. Maelezo ya picha yalisema: Picha hiyo ilipigwa katika kituo cha Jeshi la Anga cha Aviano, eneo la Pordenone, nchini Italia.
Hatimaye, picha ya nne ilichapishwa mwaka wa 2024, na utangulizi huu:
“Kuanzia tarehe 18 hadi 20 Mei 2024, muungano wa Nord Cotentin Mémoire 1944 ukiandaa toleo la tatu la kambi ya kuigiza matukio ya kihistoria ya Vikosi vya Washirika (Allied forces) huko Virandeville.”
Hadi tukichapisha ukaguzi huu hakuna taarifa rasmi kutoka Burundi, DRC au Marekani iliokuwa imetangaza kupelekwa kwa vikosi vya Marekani au vifaa nchini Burundi.
Vyanzo vyetu kule Bujumbura vimetuarifu kuwa kwa sasa hakuna vikosi wala vifaa vya Marekani vilivyopelekwa nchini humo kwa ajili ya kupelekwa baadaye nchini DRC.
14 août 2026
Swahili (generic)
9 Mo