Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:02
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Mnamo mwezi Mei 2026, mamlaka za afya zilitangaza mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundi’ bugyo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda, huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likisema hii ni dharura ya afya ya umma ya kimataifa.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka WHO, aina hii ni miongoni mwa virusi vinavyohusika na janga la Ebola, na kwa sasa hakuna chanjo iliyoidhinishwa inayopatikana au tiba mahususi iliyoidhinishwa.
Kutokana na janga hili, machapisho kwenye TikTok, Facebook, na WhatsApp yanadai kuna mbinu za kuzuia au kutibu Ebola. Video moja kwenye Tiktok ya Mei 18, inapendekeza mchanganyiko wa majani ya mpera, mdalasini, karafuu, vitunguu nyekundu, hibiscus na pilipili nyeusi, kuchemshwa kabla ya kutumika, hata kwa watoto.
Madai kuwa kuna tiba asili ya Ebola nchini DRC
Kutokana na athari za kueneza habari potofu wakati wa janga, tunaanza kuhakiki dai hili. Matokeo yanaonesha hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha ufanisi wa maandalizi haya; kinyume chake, matumizi yao yanaweza kusababisha madhara zaidi.
Tumefanya ukaguzi ili kupata maarifa ya kisayansi kuhusu maandalizi ya kitamaduni au chai hii inayowasilishwa kwenye mitandao ya kijamii kama tiba dhidi ya Ebola. WHO haijaidhinisha matumizi yoyote ya maandalizi haya dhidi ya Ebola.
Akitoa maelezo mafupi kuhusu Ebola mnamo Mei 19, katika matangazo ya moja kwa moja kwenye chaneli ya YouTube, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba ya Biolojia, Jean-Jacques Muyembe Tamfum, alisema aina hii ya virusi bado inaendelea kufanyiwa utafiti.
Soma piaDRC: Serikali yaimarisha juhudi za kupunguza kuenea kwa Ebola
Pia mkurugenzi mkuu wa Afrika CDC, Jean Kaseya, alithibitisha ukosefu wa sasa wa zana maalum za matibabu dhidi ya aina hii. Katika mahojiano na TV5 Monde mnamo Mei 17, alisema:
"Ninathibitisha kuwa tofauti na ile ya Zaire, hatuna chanjo wala dawa."
Taasisi za kisayansi ikiwemo WHO, INRB, na Africa CDC, zinathibitisha kuwa kwa sasa hakuna chanjo iliyoidhinishwa au matibabu mahususi yaliyoidhinishwa kwa aina ya virusi vya Bundibugyo.
Madhara ya hivi karibuni tumeshuhudia kutokana na habari potofu haswa kuhusu Ebola, ni vijana kuchoma kituo cha Ebola huko Rwampara, walioshuhudia wakisema wanaondesha kituo hicho walituhumiwa kusema uwongo kuhusu Ebola.
Soma piaRDC: Eneo maalum la wagonjwa wa Ebola laharibiwa Rwampara
Hivi ndivyo mamlaka za afya zinasema, habari za uwongo zinapoenea kwa haraka, huchochea magonjwa ya mlipuko kwa kuhimiza tabia hatari, kama vile kupuuza ushauri wa matibabu, na kudhoofisha majibu ya afya ya umma, na hivyo kuchelewesha juhudi za kuzuia maambukizo.
30 mai 2026
Swahili (generic)
9 Mo