Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:56
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Moja ya habari tunayoangazia ni video inayodaiwa ni waziri wa afya wa Uganda Dr. Ruth Jane akitangaza kufungwa kwa shule kutokana na Ebola.
Nchini Uganda, wiki hii matukio 15 ya Ebola aina ya Bundibugyo yameripotiwa na kifo kimoja, maeneo yaliyoathirika yakiwa Kampala na Wakiso. Mikakati mbalimbali imewekwa kudhibiti virusi hivi.
Kutokana na mlipuko huu, video kwenye Tiktok inadai inamuonyesha aliyekuwa Waziri wa Afya, Dk Jane Ruth Aceng akitangaza kufungwa kwa shule zote. Video ilichapishwa kwenye akaunti inayoitwa "Ur Uganda."
Kufuatia mlipuko huu, serikali ilitoa Taratibu za Uendeshaji Kawaida wakati shule zilikuwa zinafunguliwa kwa muhula wa pili tarehe 25 Mei 2026. Wizara ya Afya ilishikilia kuwa shule hazingefungwa.
Lakini, je serikali imebadilisha msimamo na kutangaza kufungwa kwa shule? Hakuna ripoti ya vyombo vya habari au mawasiliano rasmi yanayothibitisha hili. Uchunguzi zaidi umebaini Dkt. Ruth si tena Waziri wa Afya nchini Uganda, kufuatia mabadiliko ya baraza la mawaziri Mei 2026.
Uhakiki wa karibu wa video unaashiria kuwa hotuba inaonekana kutokuwa ya kawaida, na mara nyingi hili linapotokea ni ishara kuwa maudhui yanatokana na Akili Unde ukipenda AI.
Pia tukitumia mbinu ya Reverse Image Search, ya picha ya skrini kutoka kwenye klipu, matokeo yanatuletea picha za zamani zake Dr. Ruth akihudhuria mkutano wa ukaguzi wa 2024 huko Munyonyo.
Mandharinyuma yanalingana kwa karibu na yale ya video inayochunguzwa, na kupendekeza kuwa picha za tukio la 2024 zilibadilishwa kidijitali kuunda klipu hiyo ghushi.
Mnamo Juni 2, 2026, waziri wa elimu ya juu, Dr. John Chrysostom Muyingo, alionya umma dhidi ya habari potofu zinazoenezwa na wanablogu wa mitandao ya kijamii.
Waziri Muyingo, amesema klipu zinasamabazwa kwa kutumia sauti na vídeo za zamani. Msikilizaji vídeo ya Tiktok inayodai Uganda imetangaza kufunga shule kutokana na mlipuko wa Ebola, ni ya uongo.
05 juin 2026
Swahili (generic)
9 Mo