Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Kuna picha moja ninayoitazama hapa kwenye mtandao wa X inawaonyesha wanasiasa wa Kongo, Martin Fayulu na Joseph Kabila, wakiwa pamoja. Baadhi ya watu wameiwasilisha kama ushahidi wa mkutano wa ana kwa ana, walakini picha hiyo imetengenezwa kwa kutumia akili Unde (AI).
Julai 6, akaunti moja ya X ilichapisha picha hiyo na maandishi yanayosema
“Tuliposema kuwa upinzani huu uko chini ya udhibiti wa Kanambe, maarufu Kabila, wengine walituona watu wasiojua wanachosema. Sasa leo, fursa imepatikana ya kuweka mambo wazi.” Aliendelea kusema kuwa Fayulu amejiunga na Kabila.”
Sasa katika uchunguzi wetu tulifanya utafutaji wa picha kwa kutumia Google Lens na Search by Image, utafiti haukuonesha picha halisi inayolingana na picha hii; haukuonehsa chapisho rasmi, wala ripoti kutoka chombo cha habari kinachoaminika inayothibitisha kuwepo kwa mkutano kati ya Martin Fayulu na Joseph Kabila mwezi Julai mwaka 2026.
Pia tuliuliza Google swali hili: "Je, kulikuwa na mkutano kati ya Fayulu na Kabila?" Maelezo yake ni: "Hakujawa na mkutano wa ana kwa ana uliothibitishwa hivi karibuni kati ya hao wawili."
Pia tuliangalia vyanzo vingine huru, ikiwa ni pamoja na taarifa za umma na ripoti za vyombo vya habari zilizopo. Hakuna ushahidi uliopatikana kuthibitisha kwamba mkutano unaolingana na picha hii ulifanyika.
Uchambuzi wa picha unaonyesha dalili kadhaa za picha zinazozalishwa na AI. Mikono na vidole vinaonyesha maumbo yasiyo ya kawaida na maelezo ya anatomia yasiyolingana.
Hati inayoonyeshwa ukutani ina maandishi yasiyosomeka na kasoro hizi huonekana mara kwa mara katika picha zilizoundwa kupitia AI. Jupiter picha hizi zimetolewa wakati huu hali ya kisiasa nchini DRC ni tete. Rais wa zamani wa Kongo, Joseph Kabila, anakabiliwa kisheria.
Wakati huo huo, viongozi kadhaa wa upinzani nchini Kongo, akiwemo Martin Fayulu, wameongeza kasi ya jitihada za kisiasa kuhusiana na suala la mazungumzo ya kitaifa na hali ya usalama.
Utakumbuka mnamo Julai 6 siku ya kusambazwa kwa picha hii, viongozi wa upinzani walisafiri Burundi na kukutana na rais Évariste Ndayishimiye. Hata hivyo, muktadha huu hautoi uthibitisho wa mkutano kati ya Fayulu na Kabila kama inavyodai picha kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya kuchunguza hii picha, imebainika kuwa si halisi na haionyeshi mkutano kati ya Martin Fayulu na Joseph Kabila. Ni maudhui yaliyotengenezwa kwa kutumia akili Unde, AI na kusambazwa katika muktadha wa kisiasa nchini DRC.
10 juillet 2026
Swahili (generic)
9 Mo