Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:08
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Tarehe 12 Julai, hati bandia iliyohusishwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) ilisambazwa kudai kutangaza kuwa Senegal imetunukiwa ushindi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2026. Hata hivyo hakuna taarifa kama hiyo.
Chapisho kwenye Facebook linadai “Senegal imetetea taji lake kama mabingwa wa Afrika!" Watumiaji wengi wa mtandao nchini Senegal tangu wikendi iliyopita, wamekuwa wakidai kwamba 'Simba wa Teranga' wametangazwa kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika la mwaka 2025, baada ya kuifunga Morocco, timu waliyokutana nayo katika fainali.
Hati hii ambayo kwa kiasi fulani inatumia muundo wa Mahakama ya CAS, inaeleza kuwa timu ya Senegal "imethibitishwa kuwa mshindi" wa AFCON. Hata hivyo, hati hiyo ni ghushi. Hakuna uamuzi wowote ambao umefanywa na CAS kuhusu suala hili.
Aidha, hati hiyo ghushi inatumia namba ya kesi (2026/A/10857) ambayo si namba inayotumiwa na CAS katika mzozo huu. Namba husika ni 2026/A/12295, kulingana na tovuti kadhaa za uchambuzi wa kisheria.
Madai haya yamesababisha vyombo vingi vya habari vya Morocco na Senegal kuhakiki taarifa hii, wakati huu shirikisho la soka la Morocco liliambia chombo cha habari cha Morocco, Hespress, kwamba halikuwa limepokea "uamuzi wowote kutoka kwa Mahakama hiyo.
Hii si mara ya kwanza uvumi kama huu kusambaa, Mwezi Mei, taarifa bandia kwa vyombo vya habari kutoka kwenye taasisi hiyo — ambayo ilihusisha ushindi na Senegal ilichangia kuchochea mkanganyiko na mivutano iliyozunguka fainali hii ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Hata hivyo hakuna taarifa kama hii kutoka Mahakama ya usuluhishi wa michezo, CAS. Mapema mwezi huu, Kamati ya Rufaa ya CAF iliipa Morocco ushindi kwa kuzingatia vifungu vya 82 na 84 vya kanuni za mashindano, licha ya Senegal kushinda mabao 3 bila dhidi ya Morocco.
Vipengele hivi vinaelekeza kuwa timu yoyote "itakayokataa kucheza, au kuondoka uwanjani kabla ya kumalizika kwa muda rasmi wa mchezo bila ruhusa ya mwamuzi, itachukuliwa kuwa imeshindwa"
Utakumbuka baadhi ya wachezaji wa Senegal waliondoka uwanjani kupinga maamuzi ya mwamuzi, hasa kuipa Morocco penalti. Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi sinayotangaza Senegal kuwa washindi wa AFCON.
18 juillet 2026
Swahili (generic)
9 Mo