Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Wiki hii tunaulizana je ni kweli Joseph Kabila alikuwa Rwanda mwezi Aprili mwaka huu?
Katika mitandao ya kijamii habari ni nyingi, na baadhi yazo ni za kupotosha. Tuchukulie mfano wa nchi ya Jamhuri ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, video inadai kumuonyesha rais wa zamani Joseph Kabila katika safari ya kidiplomasia nchini Rwanda mwezi Aprili 2026, ili kutafuta amani.
Kujibu uvumi huu, tumetafuta kupitia mbinu ya Reverse Iamge Search, lakini pia kuangalia kwenye kumbukumbu za vyombo vya habari vinavyoaminika, picha hizi ni za Agosti 2016, wakati wa mkutano wa kilele wa nchi mbili huko Rubavu, Rwanda.
Video hiyo iliyotumwa mtandaoni tarehe 4 Aprili, inamuonyesha Kabila akipokelewa na timu ya Paul Kagame nchini Rwanda. Nukuu kwenye video iansema "Joseph Kabila aliwasili Rwanda, kutafuta amani DRC."
Watumiaji mbalimbali walitoa maoni kinzani, mmoja aliandika "Tshisekedi pia alipokelewa vyema,"mtumiaji mwingine akapinga, akisema: "Picha ni ya zamani."
Baada ya uchunguzi wa karibu wa ushahidi wa kidijitali, picha inayozunguka ikiashiria ni ya hivi majuzi, imetumika katika muktadha tofauti na machapisho mbalimbali yanaweza kuthibitisha hili.
Kwa mfano kumbukumbu ya machapisho kwenye vyombo vya habari vya kuaminika, kama vile nakala iliyochapishwa na Sauti ya Amerika na 7sur7, inathibitisha bila shaka kwamba picha hizi na video kweli ni ya tarehe 12 Agosti 2016.
Makala nyingine, iliyochapishwa na Beto.cd na yenye jina la "Joseph Kabila in Rwanda: zinathibitisha hili. Wakati huo, Rais wa zamani wa Kongo Joseph Kabila alisafiri kutoka Goma hadi Rubavu kwa ziara ya kikazi ya siku moja kukutana na mwenzake, Paul Kagame.
Maudhui ya wavuti wa Beto yanathibitishwa na ripoti za kina kutoka kwa Jeune Afrique na RFI za tarehe 12 Agosti 2016, zilizoandika kuhusu mkutano wa saa 24 uliofanyika miaka kumi iliyopita kati ya viongozi hao wawili.
Pia, kwenye tovuti ya habari ya mtandaoni Media Congo, tulipata taarifa ya pamoja iliyotiwa saini mnamo Agosti 12, 2016. Taarifa hiyo inataja kuwa majadiliano yalilenga katika maslahi ya pamoja ya kimkakati, ikiwa ni pamoja na biashara ya mipakani, miradi ya nishati kama vile unyonyaji wa gesi ya methane katika Ziwa Kivu.
Uhalisia ni kuwa video inayomuonyesha Joseph Kabila akiwa Rwanda, lakini sio ya mwezi Aprili mwaka huu bali ni tukio la kidiplomasia la miaka kumi iliyopita, huko Rubavu, Rwanda.
Hadi sasa, hakuna safari rasmi au ya kibinafsi ya rais wa zamani wa Kongo kwenda Rwanda iliyorekodiwa mwaka huu 2026.
01 mai 2026
Swahili (generic)
9 Mo