Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:57
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026 inaendelea, ilianza Juni 11. Waandaaji ni Marekani, Mexico na Canada. Timu 10 kutoka Afrika zinashiriki na la kupendeza zaidi, Afrika imewakilishwa na timu ya DRC.
Katika muktadha huu, video kwenye Youtube ina kichwa kinachosema “
“DRC kukosa Kombe la Dunia la 2026 baada ya Vizuizi Vipya vya Usafiri vya Marekani kutokana na Ebola.”
Tunachunguza ikiwa ni kweli DRC haishiriki kombe la dunia. Kwenye chaneli rasmi za Wizara ya Michezo ya DRC na Shirikisho la Soka la Kongo (FECOFA), na hakuna tangazo kama hilo la DRC kutoshiriki mashindano hayo.
Pia tumegundua kuwa, video hii ilichapishwa wiki 3 zilizopita na wakati huo, timu ya Leopards ilikuwa imeshahamisha mazoezi yao kule Ulaya Mei 2026, eneo lililotumika kama karantini ya lazima ya siku 21 nchini Ubelgiji na Uhispania kabla ya kusafiri kwenda Marekani.
Hili lilikuja baada ya Mei 22, Marekani iliweka siku 21 za karantini kwa watu wanaowasili kutoka DRC, kutokana na janga la ugonjwa wa Ebola.
Ni hatua iliyolazimu shirikisho la FECOFA kufuta mazoezi ya kule Kinshasa na kuamua kuendeleza maandalizi ya timu nchini Ubelgiji kabla ya kuondoka kuelekea Marekani.
Na kutokana na majadiliano na shirikisho la FIFA, FECOFA ilipata uthibitisho kwamba wachezaji na wafanyikazi walikuwa wakifuata matakwa yaliyowekwa na Marekani.
Video zinazodai kuwa timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) haitajumuishwa kwenye Kombe la Dunia la 2026 ni za uwongo na zimepitwa na wakati. Timu ya DRC iliwasili Houston, Texas, Juni 12 na kukaribishwa kwa mbwembwe. Ingati utakumbuka mara ya mwisho DRC kushiriki ni miaka 52 iliyopita kipindi hicho walikuwa Zaire.
Kumhakikishia msikilizaji zaidi ni kuwa, DRC wamewekwa kundi K, pamoja na Portugal, Colombia, na Uzbekistan. Siku ya Jumatano DRC walicheza na Portugal ama ukipenda Ureno na kutoka sare ya 1- 1 .Madai kuwa DRC haishiriki Kombe la dunia kutokana na Ebola ni uongo.
20 juin 2026
Swahili (generic)
9 Mo