Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Nchini Uganda, tangu uchaguzi wa rais wa Uganda wa Januari 2026, kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine alikimbia nchini humo, sasa maudhui kumhusu yameenea sana kwenye mitandao ya kijamii, hasa TikTok, kuhusu aliko.
Video ya TikTok iliyotumwa na akaunti @generalduties.media, yenye nukuu ya Luganda ikimanaanisha kwa Kiswahili "Bobi Wine amerejea Uganda" imekuwa ikisambaa.
Video inaonyesha picha za Bobi Wine akiwa amezungukwa na waandishi wa habari, akionekana kuonyesha kurejea kwake nchini Uganda.
Sasa kwa sababu dai kuhusu kurejea kwa Bobi Wine nchini Uganda lina athari kubwa za kisiasa, na video hazijataja chanzo cha kuaminika kuthibitisha kurejea kwake, kimetuchochea kuchunguza dai hili.
Uchunguzi wetu unaonesha kuwa dai hili kwenye video ya Titkok si kweli. Video imetumia picha za zamani na wala haioneshi Bobi Wine akirejea Uganda mwaka 2026.
Tulipotumia mbinu ya kuthibitisha ya Reverser Image Search, katika video hii, tulipata matokeo ya video kwenye Youtube, ya tukio lile lile, ya Septemba 20 mwaka 2018. Video inamuonesha Bobi Wine akihutubia wanahabari nyumbani kwake Magere, wilaya ya Wakiso, na si kwenye uwanja wa ndege au eneo lolote linalolingana na kurejea kwake Uganda.
Wakati huo Bobi Wine alikuwa amesafiri kwenda Marekani kupokea matibabu maalum kutokana na majeraha aliyodaiwa kupata baada ya kuteswa na maafisa wa usalama wakati na baada ya uchaguzi mdogo wa Manispaa ya Arua mwezi Agosti mwaka 2018.
Ushahidi wa msingi wa moja kwa moja kutoka kwa akaunti ya X Bobi Wine wa Mei 8, unathibitisha kuwa yeye na mkewe walikuwa wakisherehekea Siku ya Akina Mama wakiwa Michigan, Marekani. Chapisho lake lilikuja siku kadhaa baada ya video hii ya kupotosha kuchapishwa Mei 3, 2026.
Ni uongo, Bobi Wine hajarejea nchini Uganda. Bado yuko uhamishoni.
16 mai 2026
Swahili (generic)
9 Mo