Podcasts
Enjeux de société
Erdogan hints at larger nuclear partnership with Russia, unsettling Turkey's allies
10:04
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Wiki hii, tunaangazia taarifa ya tahadhari kutoka kwa Bodi ya kudhibiti dawa na Sumu kuhusu kusambaa kwa vidonge 'bandia' vya P2 nchini Kenya.
Nchini Kenya, mnamo Agosti tarehe 14, Bodi ya udhibiti wa matumizi ya Dawa na Sumu (PPB) ilibaini kundi la dawa bandia ya Postinor-2 ambayo tayari ilikuwa sokoni nchini humo, likiwa na taarifa za kupotosha kuhusu mtengenezaji wake.
Postinor-2, maarufu kama P2, ni kidonge cha dharura cha kuzuia mimba baada ya watu kujamiiana bila kinga, na kinapaswa kumezwa ndani ya saa 72 kwa mujibu wa maelezo.
Katika taarifa mpya ya tahadhari kwa umma iliyotolewa na afisa mkuu mtendaji Dkt. Ahmed Mohamed, ilielezwa kuwa dawa hizi za P2, katika vidonge vya miligramu 0.75, zilitoka katika kundi namba T34197R.
Hizi dawa zinaweza kununuliwa bila agizo la daktari, je, utazitambuaje tembe bandia za P2 zinazosambaa Kenya? Bodi hii ilifanya uchambuzi wa kulinganisha kati ya dawa bandia na zile halisi zinazotengenezwa na kampuni ya Gedeon Richter Plc, na kubaini tofauti kadhaa zinazoonekana wazi katika mbinu za uchapishaji wa taarifa za kundi la uzalishaji.
Pia waligundua kuwa kijitabu cha maelezo kwa mgonjwa kilikuwa na makosa kadhaa ya uchapishaji na ya kiuandishi. Namna ya kufunga katoni ni tofauti na ile ya bidhaa halisi. Katika taarifa ya tahadhari kwa umma, Dkt. Ahmed alisema namnukuu: "Pakiti halisi za Gedeon Richter hufungwa kwa kutumia njia ya gundi inayoyeyushwa na joto, ilhali pakiti bandia ilikuwa tofauti.”
Bodi ilibainisha sehemu nyingine za kifungashio za kundi la dawa ghushi zilikuwa na rangi nzito zaidi ikilinganishwa na bidhaa halisi. Kiashiria cha mwisho ni maandishi kwenye nembo, ni tofauti na ile ya kifungashio halisi.
Hizi ishara zilifanya wazi kuwa dawa hizo ni ghushi na hazikutengenezwa wala kusambazwa na Gedeon Richter. Sasa hatari ya kutumia dawa hizi bandia za uzazi wa mpango za dharura kinyume cha maelezo, itakusababishia moja kwa moja kushindwa kwa njia za uzazi wa mpango na hatari kubwa za kiafya.
Nikukumbushe tu kuhusu jinsi ya kutambua Postinor 2 ambayo ni bandia. Rangi ya chungwa kwenye jina la bidhaa na kifungashio huwa imekolea zaidi kwenye bidhaa hiyo bandia.
Kundi la dawa bandia linaonyesha kutofautiana katika mbinu za uchapishaji wa nambari za kundi, makosa ya uchapaji katika kijikaratasi cha taarifa za mgonjwa, na fonti zisizo sahihi za nembo. Imethibitishwa wazi kuwa vidonge vya Postinor-2 (hasa vile vya Kundi Nambari T34197R) nchini Kenya ni ghushi.
Wataalamu wa afya wanatoa onyo kali kwamba P2 ni dawa ya dharura ya kuzuia mimba na haipaswi kutumiwa kama njia ya kawaida ya uzazi wa mpango.
21 août 2026
Swahili (generic)
9 Mo