Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
19:56
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Nairobi ni mwenyeji wa msitu mkubwa wa mvua ulio salama ndani ya mipaka yake: Hifadhi ya Karura yenye ukubwa wa hekari 1,000 ni mapafu muhimu ya mji mkuu wa Kenya, katika kuchuja uchafuzi wa mazingira kwa mamilioni. Ilikuwa ishara ya ukosefu wa usalama, sasa ni mfano mkuu wa kimataifa wa uhifadhi unaoongozwa na jamii haswa shirika la marafiki wa Karura maarufu Friends of Karura.
Hata hivyo, msitu wa Karura unakabiliwa na changamoto za kina za kiikolojia. Miti ya kigeni inayokua haraka, uchafuzi wa mazingira wa mijini, magugu vamizi, na kuingiliwa kwa minajili ya upanuzi wa barabara na ujenzi wa miundombinu.
Ili kukabiliana na hili, juhudi kubwa za urejesho zinaendelea. Mpango wa utaratibu wa asilimia 60 unaendelea ili kubadilisha miti isiyo ya asili na spishi za urithi katika kurejesha udongo na bioanuwai.Urejeshaji huu unaoendelea hutumika kama mwongozo wa jinsi miji ya kisasa inaweza kurekebisha urithi wao wa asili.
21 mai 2026
Swahili (generic)
18 Mo