Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:13
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Watu wengi wanapokaribia kufunga ndoa,hujukumika kufanya vipimo vya virusi vya HIV .Wengi hufanya kipimo hicho si kwa sababu wanajua umuhimu wake bali ni kwa sababu ya ulazima kabla kufunga harusi haswa za Kikristo.
Hata hivyo watalaam wa afya wanasema kuna vipimo tele ambavyo ni muhimu pia na vinahitajika kufanywa kabla ndoa.
Mwanasaikolojia Naomi Ngugi anasema kando na kipimo cha HIV,kuna kipimo cha Rhesus Factor ambayo kama mtu na mwenzake hana ufahamu ,wanaweza kupata shida ya kuharibika mimba.
Kuna pia kipimo cha Genotype kubaini uwepo wa ugonjwa kama Selimundu ,Hepatitis B, Hepatitis C au homa ya ini,vipimo vya Magonjwa sugu, Magonjwa ya akili na Vipimo vya uzazi kubaini ubora wa mbegu za kiume na matatizo ya mirija kuziba upande wa wanawake.
Vipimo hivyo vinaweza kugharimu ndoa iwapo wanandoa hawataweka wazi.
24 septembre 2025
Swahili (generic)
9 Mo