Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Licha ya makubaliano ya Washington yaliyotiwa saini mwezi Disemba 2025 kati ya DRC na Rwanda, pamoja na usitishaji mapigano uliohitimishwa kati ya serikali ya Kongo na waasi wa AFC/M23, eneo la mashariki ya Congo halionekani kupata amani ya kudumu katika siku za hivi karibuni.
Mapigano ya mara kwa mara yanaendelea na kutokana na hili kuna minong'ono mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uungwaji mkono wa madola ya kigeni kwa majeshi ya Kongo, kwa lengo la kuyateka upya maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa waasi na washirika wake.
Ni katika muktadha huu ambapo taarifa tunazozithibitisha zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii haswa kwenye Facebook na X. Moja kwenye Facebook inasema na ninanukuu
"Kulingana na chanzo, wanajeshi wa Israel wametumwa mashariki mwa Kongo. Dhamira yao ni kuchangia kukomboa Bukavu. “
Tunaanza kwa kutafuta kwenye Google kwa kutumia maneno muhimu kama vile "Wanajeshi wa Israeli, wametumwa, Kongo Mashariki, Bukavu" ili kuthibitisha uhalisi wake.
Kutokana na matokeo ya kwanza kabisa, tuligundua kuwa hakuna chanzo kinachoaminika, rasmi au kinachohusiana na vyombo vya habari, kingeweza kuthibitisha madai haya.
Tunaangalia zaidi njia rasmi za mawasiliano za Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) na IDF, jeshi la Israeli. Kwa pande zote mbili, hatukupata taarifa zinazoonyesha ushirikiano wowote wa hivi majuzi kati ya vikosi vya Kongo na Israel mashariki mwa DRC.
Tuliangalia kwenye akaunti ya X ya msemaji wa kundi la AFC/M23 ili kuona taarifa yoyote kushtumu hili, na hatukupata taarifa kama hiyo.
Habari pekee tulipata inayohusiana na hili ni chapisho lililotaja ziara ya Rais wa Israeli Isaac Herzog kule Kinshasa mnamo Novemba 2025, suala la kutumwa kwa jeshi halikutangazwa.
Je, tunajua nini kuhusu ushirikiano wa kijeshi wa DRC na Israel? Kimsingi inahusu programu za mafunzo, bila ushahidi wa kuwepo au kutumwa kwa wanajeshi wa Israel ardhini nchini DRC. Hakuna ushahidi wa kuunga mkono madai kwamba wanajeshi wa Israel wametumwa mashariki mwa DRC.
Hadi sasa, habari zinazohusisha jeshi la Kongo na Israel zinataja tu ushirikiano kulingana na mafunzo na kujenga uwezo kwa jeshi la FARDC. Pia tumewasiliana kwa njia ya simu na ubalozi wa Israeli jijini Nairobi, na wakajibu hivi na nanukuu “Jeshi la Israel halijatuma wanajeshi DRC.”
04 avril 2026
Swahili (generic)
9 Mo