Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:58
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Nchi ya Ufaransa imelitambua taifa la Palestina na sasa kuna video ya uongo inayodai kuwaonyesha wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina wakitishia kuibadilisha Ufaransa kuwa taifa la Kiislamu. Hii ni propaganda.
Video hii ya sekunde 23 inawaonyesha wanaume watatu, nyuso zao zikiwa zimefunikwa na kitambaa ambacho kawaida hupatikana katika maeneo kame, ili kujikinga dhidi ya kuchomwa na jua, vumbi, na mchanga.
Video hii ilichukuliwa mbele ya ukuta uliopambwa kwa bendera ya Palestina. Mtu aliye katikati akionekana kuwa na kisu mkononi, anaongea Kiarabu akitishia kwamba “atabadilisha Ufaransa kuwa taifa la Kiislamu”.
Kitengo cha kuhakiki cha RFI kiligundua video hii inafanana zingine za zamani. Moja, ni ya Julai 2024, ilidai kuonyesha mwanachama wa Hamas akitishia kufanya mashambulio wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Paris.
Ya pili, ya hivi majuzi zaidi, ilipaswa kuonyesha wanajihadi wakitishia kuchoma moto Kanisa Kuu la Notre-Dame huko Paris. Uwepo wa wanaume waliovalia kofia, ukuta wa zege, uigizaji, na mazingira yote hayaendani.
Kulingana na tafiti mbalimbali, video hizi ni sehemu ya operesheni kubwa ya upotoshaji ya Urusi inayoitwa Storm-1516. Kampeni yenye malengo kadhaa ikiwemo kukashifu Ukraine, kukashifu sera za Magharibi, lakini pia kuvuruga mijadala ya umma kwa kuhusu mada kama vile uhamiaji na ugaidi.
Katika ripoti yake, kitengo cha kiufundi na uendeshaji cha Ufaransa cha Viginum, kinazingatia kuwa shughuli za Storm-1516 "zinawakilisha tishio kubwa nchini Ufaransa na katika nchi zote za Ulaya."
Pia tulichanganua muundo wa usambazaji wa akaunti hii. Video ilionekana kwa mara ya kwanza kwenye X mnamo Septemba 14, 2025, saa kumi na moja na dakika sita jioni kwenye akaunti ya lugha ya Kiarabu iliyoundwa Septemba 2012. Hizi ndizo picha pekee ambazo amechapisha kufikia sasa.
26 septembre 2025
Swahili (generic)
9 Mo