Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
10:00
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Moja ya habari ya kupotosha ambayo tunaangazia ni madai ya mpango wa uwekezaji mtandaoni unaohusishwa na Wizara ya Fedha nchini DRC.
Tuanze kuangazia habari kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ya Julai mosi, ambayo imekuwa ikienea mitandaoni ikiwapotosha raia kwamba Wizara ya Fedha nchini humo imeanzisha mpango wa uwekezaji mtandaoni.
Maudhui ya waraka huo yenye nambari ya kumbukumbu 005 yanasomeka “Wizara ya Fedha inautaarifu umma kuhusu uzinduzi rasmi wa uwekezaji mtandaoni, ulioanzishwa kufuatia kupitishwa kwa bajeti ya taifa ya mwaka wa fedha wa 2025.”
Hati inaendelea kusema “Mpango huu unalenga kuwapa wananchi fursa rahisi, ya haraka na inayofikiwa, na uwezekano wa kuzalisha faida ndani ya saa 2 na dakika 30 tu baada ya kuwekeza.”
Kadhalika hati inaeleza "Programu inaungwa mkono na wataalam waliobobea katika teknolojia ya dijiti, hivyo basi kuhakikisha mazingira salama na miamala ya haraka kwa washiriki wote." Kisha inatoa maelekezo ya mahitaji ili kushiriki ikiwemo: "Picha ya mwekezaji, nambari ya simu ili kupokea pesa za ushindi; Kiasi unachotaka kuwekeza."
Utaratibu wa malipo: Malipo hufanywa pekee kupitia akaunti yako ya M-PESA au AIRTEL MONEY, itakayotumwa kwako moja kwa moja na timu rasmi ya usaidizi ya WhatsApp. Hakuna linki ya nje au tovuti zinazohitajika. Malipo yanachukuliwa kuwa halali tu baada ya kuthibitishwa na usaidizi wa WhatsApp kwa nambari ambayo naona imechapishwa hapo.... (+243) 832 650 566.
Kadhalika taarifa hii inaeleza kuwa agizo hili litaendelea kuwepo hadi pale uamuzi mpya utakapotolewa na Wizara, ambayo kwa mujibu wa hati hiyo, inawashukuru washirika kwa imani na mchango wao katika ukuaji wa uchumi
Hata hivyo msikilizaji hati hii ni ya uongo. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Julai 7, Wizara ya Fedha ilikanusha uhalisi wa hati iliosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Katika taarifa hii kwa vyombo vya habari kwenye akaunti yake rasmi ya Facebook inasema "Hati hii ni ya uongo. Wizara haikuanzisha au kufadhili operesheni kama hiyo."
Wizara hiyo ya fedha ya DRC ilitoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu ikiwakumbusha kuwa taarifa zote rasmi huchapishwa kupitia njia zake za mawasiliano zinazotambulika pekee.
Tuliwasiliana na Wizara ya fehda ya kongo kwa njia ya simu na hata kutuma ujumbe kwa njia ya Whatsaap ambapo waliahidi kuzungumza nasi ila hadi tukirusha kipindi hiki hewani, maofisa husika hawakuwa wamerejea kwetu.
19 juillet 2025
Swahili (generic)
9 Mo