Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:59
Swahili (generic)
Podcasts
2026
Wakati huu bado suluhisho likiendelea kutafutwa na washikadau wa ndani lakini pia kimataifa kuhusu mzozo wa Congo, taarifa ghushi, na zinazopotosha zinaendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Barua imekuwa ikisambazwa ikidai kutoka kwa ofisi ya msemaji wa Serikali kuhusu Rwanda, kwamba Rais Kagame hajui kinachoendelea mashariki mwa DRC.
Barua hii ilisambazwa kwenye Facaebook kwa Kinyarwanda, chapisho lingine kwa Kifaransa na pia kuna chapisho kwenye X, Ingati hii barua feki inaanza kwa kusemaje?
Aya ya kwanza inasoma,
"Rais Paul Kagame anasikitika kuwafahamisha Marekani, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, na washirika wake wengine kwamba hakuwa na habari kuhusu migogoro inayoendelea DRC. Ni siku chache tu zilizopita alijulishwa."
Kisha barua hii feki inamaliza kwa kusema
"Rais anawahakikishia washirika wake kwamba sasa anafahamu, atachukua hatua kwa dhamira kukomesha kile ambacho alikuwa hajui."
Tunaanza kuchunguza. Mtumizi mmoja kwenye X alikanusha barua hiyo
“Kama ujanja ungekuwa ustadi, hii bado ingefeli misingi. Ni dhaifu, mantiki dhaifu, haina maana kabisa."
Tuliangalia akaunti rasmi za Rwanda na hatukuona barua kama hiyo. Mitandaoni tumekutana na barua zingine za ucheshi ambazo zimesambazwa hapo awali ili kupotosha umma.
Sasa je barua hii ni halali? Katika uchanganuzi wetu, barua hiyo inaonyesha taarifa ya kejeli kwa vyombo vya habari kutoka kwa "Ofisi ya Msemaji wa Serikali ya Rwanda" ya Februari 6, 2026. Muktadha wa ujumbe huo ni kazi ya kejeli na sio taarifa rasmi ya serikali.
Tunalinganisha barua hiyo na barua rasmi kutoka ofisi ya msemaji wa Serikali ya Rwanda, kwa uangalifu barua ya uwongo, maandishi hayaonekani vizuri, maneno yameongezwa juu. Pia barua rasmi kutoka Rwanda inatumia rangi ya bluu na nyeusi kinyume cha rangi zilizoko kwenye barua feki.
Kulingana na shughuli za hivi majuzi za kidiplomasia, dhamira ya machapisho ya hivi majuzi ya kejeli, makali au ya uchokozi yanayodai kuwa yanatoka Rwanda ina nia ya kubadilisha mtazamo wa mzozo wa DRC.
Habari hii pia ilisambazwa mwezi baada ya rais Paul Kagame, kuzungumza kwenye Baraza la 20 la Mazungumzo ya Kitaifa, akigusia changamoto zinazoendelea za usalama wa kikanda, haswa kukosekana kwa utulivu mashariki mwa RDC.
20 février 2026
Swahili (generic)
9 Mo