Podcasts
Enjeux de société
An be kuma kankɔnɔdiimibana "diphtérie" de kan bi o min be ka ye Sénégal, Mauritanie ani Nigéria
9:59
Swahili (generic)
Podcasts
2025
Tunaangalia barua inayodai DRC imeipa Rwanda makataa ya siku tisini kutekeleza makubaliano ya amani ya Washington.
Tuanze kwa kuangalia masuala yanayohusiana na mkataba wa amani kati ya DRC na Rwanda. Mnamo Juni 27 pande hizo mbili zilisaini makubaliano ya amani chini ya upatanishi wa Marekani jijini Washington.
Siku kadhaa baadaye, mnamo July 6, kuna barua iliyoenea mitandaoni ikidai utawala wa DRC umeipa Rwanda makataa ya miezi mitatu kutekeleza makubaliano yaliyoongozwa na Marekani.
Sehemu ya barua hiyo inasema
“Baada ya kipindi hiki, DRC itakuwa na haki ya kukamata tena Goma, Masisi, Minova, Bukavu, Kamanyola, Luvungi, na maeneo mengine yoyote yanayokaliwa kwa mabavu. Ikiwa tishio hilo litaendelea, linaweza pia kushambulia ngome yoyote ya adui nje ya mipaka yake, ikiwa ni pamoja na katika ardhi ya Rwanda."
Tunajiuliza je barua hii ni halali? Tumeangalia kwenye mitandao rasmi ya serikali ya Kinshasa na hakuna mawasiliano kama hayo.
Pia mpangilio wa vipengele vya hati, ni kidokezo kingine kinachothibitisha kuwa barua hii ni bandia.
Barua hii imendikwa “Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Msikilizaji ukichunguza kwa makini, Waraka rasmi kama huu wa serikali ya Kongo una nembo upande wa kushoto na upau wa bluu, njano na nyekundu, unaotenganisha maneno ya Wizara ya Mawasiliano na Vyombo vya Habari yaliyoandikwa kwa herufi kubwa.
Kwa upande mwingine, kwa barua tunayoichunguza, nembo iko katikati, chini yake imetajwa "Wizara ya Mawasiliano na Vyombo vya Habari" kwa herufi ndogo ikifuatiwa na saini "Waziri" na tarehe.
Mtindo uliotumika unafanana na waraka wa ripoti ya Baraza la Mawaziri na si ule unaotumika na wizara hiyo. Pia akaunti ya mwandishi mmoja wa habari aliyechapisha barua hiyo baadaye alisema ilikuwa feki.
Naye msemaji wa serikali ya RDC, Patrick Muyaya kupitia X aliandika haabri hiyo si kweli. Nimnukuu “Waraka huu si skweli. Hebu iondoe mtandaoni. Jizuie kueneza uchafu huu
Ripoti ya hivi punde ya serikali ya Kongo haikutaja masharti haya ya DRC kwa Rwanda. Pia barua hii haijachapishwa kwenye tovuti yao wala katika vyombo vya habari vya Kongo.
12 juillet 2025
Swahili (generic)
9 Mo